Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya
Tanzania na Lesotho unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 10, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi
wa kati wakati wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth
wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda
huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia
Waamuzi
hao pamoja na kamishna wanatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania
kesho Ijumaa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) wakati
wapinzani wa Taifa Stars wanaingia jioni ya saa 11.55 kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Afrika Kusini. Timu hiyo itafikia Hoteli ya Southern
Sun, Dar es Salaam.
Mchezo
kati ya Taifa Stars na Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku
kwenye Uwanja wa Azam uliko Chamazi, Dar es Salaam na ili kuwapa fursa
Watanzania wengi kushuhudia mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limeondoka kiingilio cha Sh 15,000.
Hivyo sasa Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.
Kujiandaa
na Mchezo huo Taifa Stars ilipiga kambi hapa nchini kuanzia Mei 23,
mwaka huu kabla ya kwenda Alexandria, Kaskazini kabisa mwa nchi ya Misri
ambako ilipiga kambi ya wiki. Kambi hiyo ilifurahiwa na Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Salum Mayanga.
Mchezo
huo dhidi ya Lesotho utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi
‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya
Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Mbali
ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na
Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa
katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
EmoticonEmoticon