Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza
jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali,
kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga,
katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini
Dodoma.
Viongozi
waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika
la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada
ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha
2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango, mjini Dodom
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia
jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi
Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida
katika mwaka wa fedha 2016/2017
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza
jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi
Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida
kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango Mjini Dodoma
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akitoa neno la
Shukrani kwa uongozi Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ubunifu na
uwajibikaji wao ulioliwezesha Shirika hilo kupata faida na kutoa gawiwo
kwa Serikali, Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………….
Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
SERIKALI
imeendelea kupata neema kutokana na uwekezaji wake kwenye mashirika na
taasisi mbalimbali yanayojiendesha kibiashara nchini ambapo leo Shirika
la Bima la Taifa (NIC) limetoa gawiwo la Shilingi bilioni 1.707 baada ya
kupata faida kiabishara mwaka 2016/2017.
Kwa
nyakati tofauti mwaka huu, Serikali ilipokea kiasi cha Shilingi bilioni
1.7 kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kufuatiwa na NMB Bank
Plc, iliyotoa kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 hivi karibuni.
Akipokea
Hundi kifani ya kiasi hicho cha Shilingi 1.707 kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, Bw. Sam Kamanga, Waziri wa Fedha
na Mipango, amelipongeza shirika hilo kwa kuonesha maendeleo makubwa
katika kipindi kifupi tangu azindue Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo
mwishoni mwa mwaka uliopita.
“Nilipozindua
Bodi yenu ya Wakurugenzi uliniahidi Mkurugenzi Mtendaji kuwa
mtafanyakazi kwa bidii na kuanza kutoa gawiwo Serikalini, ninajisikia
furaha sana kwa niaba ya watanzania kuona kuwa mnatimiza ahadi hiyo kwa
kutoa asilimia 15 ya pato ghafi la mapato yenu. Nawapongezeni sana”
alisisitiza Dkt. Mpango.
Alizitaka
taasisi nyingine za umma zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina
zinazofikia 260 kuanza kutumia huduma za bima kupitia Shirika la Bima la
Taifa.
Alisema
anafahamu kwamba kuna taasisi nyingine zina mikataba na mashirika
mengine ya bima lakini akatoa wito kwa taasisi hizo kwamba baada ya
kumaliza mikataba yao, waanze kupata huduma kupitia NIC ambalo manufaa
yake yameanza kuonekana baada ya kuanza kurejesha sehemu ya faida yake
kwa Serikali.
Hata
hivyo Dkt. Mpango aliitaka NIC lisibweteke badala yake liboreshe huduma
zake ili kuweza kujiongezea soko kwani mashirika ya bima yamekuwa na
ushindani mkubwa.
Alilitaka
Shirika hilo kutoa elimu kwa Umma wakiwemo wakulima, wafugaji na
wananchi wengine kuhusu umuhimu wa kukatia bima mifugo, mazao, nyumba na
vyombo vya moto ili kujiepusha na hasara zinazoweza kutokea wakati wa
majanga.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) alisema kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwa Shirika hilo kutoa
gawiwo kwa Serikali tangu lianzishwe miaka 54 iliyopita na kuzitaka
Taasisi zote zilizo chini ya Wizara kuiga mfano wa NIC.
“Naamini leo ndiyo mmezaliwa na mna miaka mingine 100 mbele ya kutenda kwa ajili ya watanzania” Alisisitiza Dkt. KIjaji
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James alilipongeza
Shirika hilo na kusisitiza kuwa Wizara ipo bega kwa bega kushirikiana
nao ili kuhakikisha Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maendeleo ya
Taifa.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi hundi kifani, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima
ya Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
kwa kuzihamasisha Taasisi za Umma kukata bima NIC, na kwamba hatua hiyo
ndiyo imeliwezesha shirika kutengeneza faida na kutoa gawiwo kwa
Serikali.
Hata
hivyo ameiomba Serikali kuyahamasisha mashirika zaidi ya 200 yaliyochini
ya Msajili wa Hazina kutumia huduma za Taasisi yake ili kuongeza wigo
wa mapato na kuleta faida zaidi kwa wabia wa Shirika hilo
“Ni
Taasisi 15 tu ndizo zilizoitikia wito wa Serikali wa kutumia huduma za
bima kupitia NIC lakini mashirika na taasisi nyingine bado hivyo
ninaiomba Serikali itusaidie kufanikisha jambo hili” Alisistiza Bw.
Kamanga.
Aliiahidi
Serikali kwamba Shirika lake linatarajia kuongeza gawiwo zaidi za kiasi
hicho kilichotolewa kutokana na mikakati kabambe ya kiabiashara
waliyojiwekea.
EmoticonEmoticon