Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Bungu, wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuhusiana na masuala
mbalimbali ya kupambana na wahalifu wilayani humo. Masauni ambaye
aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro aliwataka
wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili
kuwasambaratisha wahalifu hao
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro akipokea maoni ya wananchi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani
wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi
wilayani humo. IGP ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) walizungumza
na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu kutoka Wilaya Rufiji na
Kibiti kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na
mali zao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wazee, viongozi wa
dini na watu maarufu (hawapo pichani) kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti
kuhusu masuala mbalimbali na kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi
na usalama wa raia na mali zao. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Simon Sirro, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam
Hussein.
Wazee, viongozi wa dini na wa
vyama vya siasa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao
katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kibiti, mkoani Pwani.
Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na
wananchi hao waliweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa
raia na mali zao kupitia maoni ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon