Na Honorius Mpangala.
Mchezo
wa soka ni mchezo ambao ili ufanikiwe hauhitaji jitihada za mtu mmoja
ila jitihada za timu nzima kuanzia wachezaji,viongozi na benchi la
ufundi. Klabu
ya Simba imeweza kutembea katika tafsiri hiyo ya mafanikio ya soka
yanahitaji ushirikiano wa timu nzima ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Ni
kitu ambacho wapenzi na wadau wengi wa soka hawajafahamu dhana ya
viraka vilivyopo katika mpira na mwisho vinaunda mpira mwenyewe. Viraka
vya mpira ni sehemu ya kuelezea muunganiko unaohitajika katika watu ili
kuleta mafanikio ya kitu kizima na pia utofauti wa rangi katika viraka
huelezea timu mbili tofauti katika uwanja zinazocheza mchezo wenyewe.
Msimu
wa 2016/2017 umekua bora sana kwa klabu ya simba na kufanya klabu
imalize ligi nikiwa nafasi ya pili na kufanikiwa kubeba kombe la Azam
Sport Federation Cup ( ASFC) msimu huu katika fainali Kali dhidi ya Mbao
fc ya Mwanza.
Maandalizi
ya klabu ya Simba waliyoyafanya ndiyo matunda ya walichokipata na
kitawaletea mafanikio zaidi kama wakiendekea nacho kwa misimu mingine
inayokuja.
Moja
ya eneo ambalo klabu ya simba ilikua na changamoto na kujikuta
wanashindwa kujishika vizuri ilikua katika eneo la benchi la
ufundi,naweza kusema Benchi la simba limetibiwa ipasavyo.
Joseph
Omog huyu mkameruni ni moja ya makocha wazuri na wenye kuamini katika
nidhamu ya mchezaji mmoja na baadae nidhamu ya klabu kwa ujumla. Hakuna
asiyefahamu mafanikio aliyoyapaya Omog akiwa na klabu Fc Leopard ya
Congo Brazzaville alipoifikisha katika fainali ya kombe la shirikisho
katika fainali waliyocheza dhidi ya Sc vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo.
Omog
alijitangaza katika mashindano ya afrika kama ilivyo kwa George
Lwandamina wa yanga alivyojitangaza kupitia Mashindano ya ligi ya
mabingwa. Kabla
ya ujio wa Omog klabu ya simba ilikua klabu iliyokua ikicheza soka safi
lisilo na faida kwao kutokana na upungufu wa nidhamu ya mchezo kupitia
utimamu wa mwili na kuhimili mikiki mikiki ya ligi kwa dakika tisini za
mchezo.
Omog
ni kocha mkali anayejua kusimamia nidhamu,aliondoa hali ya utoto na
kuweka mkazo wa kutafuta matokeo kwa faida ya klabu na sio mtu pekee.
Awali
ilionekana kama utani wakati simba waenda kuweka kambi yao katika
hostel za seminary pale bingwa Morogoro na kuweka mazingira ya
kujidhatiti kwa klabu.
Kulikua
na utofauti mkubwa kati ya uongozi wa benchi la ufundi chini ya Omog na
ilivyokua kwa Jackson Mayanja ambako tuliona mikwaruzano ya chini chini
kati yake na wachezaji,mfano kile kilichotokea kati ya Mayanja na
Hassan Isihaka na Hamis Kiiza.
Zoezi
la usajili walilolifanya kwa upande wa wachezaji walifanikiwa japo sio
kwa asilimia kubwa na hilo ni kutokana na aina yetu ya utafutaji wa
wachezaji wa kutoka nje ambapo walitumia majaribio.
Usajili
wa Javier Belasa Bukungu ulipondwa sana na vyombo vya habari lakini
amekuja kuwa thibtishia yeye ni mtu wa tofauti ndani ya uwanja.
Mafanikio
makubwa kwa klabu ya simba ilikua pale walipojidhatiti kuivamia mtibwa
sugar na kuwasajili Shiza Kichuya,Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim
ilikua usajili bora ambao umeleta matunda kwasababu katika mechi ya FA
Mohammed Ibrahim ndo mfungaji wa bao la kuwapeleka fainali na Kichuya
akafunga la kuipa Ubingwa wa FA achilia mbali magoli yake mawili ya
mechi dhidi ya yanga ambayo yalimtengenezea jina zaidi na zaidi Kichuya.
Wakati
ligi ikiendelea na kuona jinsi gani imekua ngumu simba walifanya makosa
ambayo hawakuyajua awali kama wanakosea, Safu ya ushambuliaji
Ikiongozwa na Laudit Mavugo ilikua inazidiwa magoli na viungo
wakiongozwa mzamiru,Mo na Kichuya huku wakiwaacha Mavugo,Fred Blagnon na
Ibrahim Ajib wakiwa na idadi ndogo ya magoli.
Simba
walimwamini sana Mavugo kuliko Blagnon kwasababu tu mienendo ya
uwanjani kati ya hawa wawili ila kiukweli mienendo ya Blagnon inafaida
zaidi kuliko Mavugo hii iko wazi ila kinacho mfanya awe nyuma ya Mavugo
ni chenga na visigino.
Nafasi
na kazi ya Mavugo na Blagnon imenikumbusha hali hiyo kwa Washambuliajj
wa kiitalia Fransisco Totti na Alessandro Del Piero. Kazi
inayoshindikana kwa Mavugo kwa kipindi cha dakika themanini kiliwezekana
kwa Blagnon kwa dakika kumi tu awepo mchezoni.
Dakika kumi za Blagnon ziliamua mechi dhidi ya mbao fc katika Michezo miwili.
Miongoni
mwa Michezo ambayo simba walitereza na kuonekana kushindwa kutegua
mitego yao ilikua dhidi ya African Lyon mchezo ambao walipoteza dakika
za mwisho za mchezo,Mchezo dhidi ya mbeya city jijini Dar es salaam
ilikua mtihani kwa klabu ya simba. Endapo benchi la ufundi likaweza
kugundua jinsi anavyocheza Mavugo katika eneo la ushambuliaji na
kumtazama Blagnon anavyocheza watakua na majibu ya maamuzi katika
kuwatumia.
Michezo
ya ugenini ambayo ilikua na wakati mgumu dhidi ya Kagera sugar,prisons
na Toto Afrika kutokana tu na kujidhatiti wakikofanya wapinzani wao na
kutengeneza woga wa safu ya ushambuliaji ya simba kwa kumpa muda mwingi
Mavugo ambaye wapinzani walishamgundua aina yake ya uchezaji.
Usajili
wa dirisha Dogo kwa kumsajili Athanas Wa stand utd haukua na tija sana
kwasababu mtu pekee alitetakiwa kupunguziwa muda wa kucheza ni Mavugo na
kupata nafasi Blagnon.
Eneo
la kiungo liko bora sana kwa viungo wa kati na tatizo linakuwa kwa
mbadala wa Ajib na Kichuya kwa viungo wa pembeni. Uwezo wa Jamal Mnyatte
na Athanas sio watu wazuri sana ambao unaweza kusema unaweza
kuwatengenezea mzunguko katika kucheza.Ndo maana Alipoyumba Kichuya
ilishindikana kwa mnyatte aliyelata nafasi ya kucheza inapobidi.
Mwinyi
kazimoto anaendelea kuwa mtu mwenye msaada sana kwa klabu katika
kutuliza munkali wa wachezaji na kutafuta matokeo unaweza kupata majibu
kwa mechi akizotokea benchi na kucheza kama ilivyo kwenye mechi ya mbao
ligi kuu.
Nafasi
ya beki simba ilifanya vyema japo Mwalimu alikua akibadilika sana
katika nafasi ya walinzi wa kati. Method Mwanjali,Juuko Murshid,Abdi
Banda, Javier Besela Bukungu, James Kotei hawa wote kwa nyakati tofauti
wamekua wakicheza nafasi hizo na kufanya mwalimu kushindwa kupata pacha
iliyo bora zaidi kwake. Majeruhi ya Mwanjali,majukumu ya timu ya taifa
ya Uganda kwa Juuko Murshid ni kati ya sababu zilipelekea kuyumba kwa
nafasi ya ulinzi na kufanya Mwalimu kufanya mzunguko kwa walinzi wake.
Nini kifanyike kwa msimu ujao.
Yapo
mambo machache ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi ndani ya klabu hiyo.
Moja, uongozi kupeana majukumu ya klabu kulingana na nafasi kiutendaji
na sio kuingiliana katika majukumu hayo kunakotoa mkanganganyiko kwa
benchi la ufundi na wachezaji pia.
Tumeweza
kujionaea klabu hiyo viongozi wake kila mmoja akitaka kuonekana sana
mbele ya vyombo vya habari na kuzungumzia klabu bila utaratibu mazuri na
kufanya kila mmoja kuonekana anajitengenezea mazingira ya kuwepo katika
nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi ujao.
Mbili,Utulivu
wa benchi la ufundi uliopo wasije kuutibua na kumfanya bundi akatua
katika paa la jengo lao kwasababu ya kutotekeleza matakwa ya kocha
baadaa ya kumaliza ligi.
Tatu,ziko
nafasi zinazogitaji marejebisho ili kufanya simba kung'ara zaidi kama
nafasi ya mlinzi wa kulia wanajitaji mtu wa kusaidiana na Bukungu
kwasababu aliyekuwepo kashindwa kumpa changamoto na nafasi hiyo itakuwa
bora sana kama wataweza kumshawishi Salum kimenya wa Tanzania prisons
kujiunga nao.
Nafasi
nyingine ambayo wanapaswa kuifanyia maamuzi ni kutazama upya nafasi ya
kiungo mkabaji toka nje ya nchi kwasababu James Kotei ameweza kufit eneo
la ulinzi kwa kucheza na Juuko hivyo kumwondoa katika mfumo Method
Mwanjali anayeonekana kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu kasi ya
ligi.
Upande
wa mlinzi wa kushoto ni eneo ambalo kwao halina matatizo kwani uwepo wa
Abdi Banda na Mohammed Hussein ni tiba tosha na kinachobaki ni kutuliza
akili zao na kutambua thamani ya mashindano wanayoshiriki hasa kwa
banda mwenye vitendo visivyo vya kiungwana mchezoni.
Kwa
upande wa nafasi ta ushambuliaji simba wana kila sababu ya kuwatazama
vizuri vijana wao waliopita klabu ya simba mbaraka Yusuph na waziri
junior,pia wana kila nafasi ya kuwatazama vizuri wachezaji kama Stamili
Mbonde wa mtibwa sugar.
Kwa
upande wa mchezaji wa nje ambaye anaweza kuondoka ni Method Mwanjali na
nafasi yake kuchukuliwa na Kotei na kufanya nafasi ya kumsajili kiungo
mkabaji wa kumpa changamoto Jonas Mkude.
@Mido sankala
EmoticonEmoticon