MD KAYOMBO ASHAURI WATANZANIA KUFUATA FURSA ZILIPO

May 29, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.

Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.

Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

Alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89

Imetolewa Na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »