Na Mwandishi Wetu, Arusha
Watumishi
wa halmashauri ya Jiji La ARUSHA Kwa kushirikana na Mkurugenzi wao
Bwana Athumani Juma Kihamia wamechangia kiasi cha shilingi Milioni 14
kwenye ibada ya harambee ya kuchangia maendeleo ya mtaa iliyofanyika
katika kanisa la KKKT usharika wa Enaboishu halmashauri ya Arusha .
Katika
Ibada hiyo ya harambee ya kuchangia maendeleo mtaa wa Loruvani ambapo
mgeni Rasmi alikuwa Mkurugenzi Kihamia amesindikizwa na watumishi pamoja
na wadau wake wa karibu wamechangia Fedha hizo kwa ajili ya kuwatia
waumini wa kanisa hilo kwa ajili ya maendeleo yao.
Ibada
hiyo ya aina yake ambayo kila Mtumishi alitoa mchango wake papo kwa
papo na wengine kwa kuahadi wamesema kuwa wamependezwa na tabia ya
Mkurugenzi wao anavyowapa ushirikiano na Moyo wa Upendo na si kazini tu
bali na nje ya kazi ndiyo mana wakamsindikiza katika ibada hiyo.
Hata
hivyo amewataka Watanzania kushirikiana katika shughuli mbalimbali za
maendeleo bila kujali dini ,kabila ,au Rangi anayotoka.
Kihamia
amesema kuwa jamii inapokuwa na ushiriano mzuri hata Mungu anawasaidia
watu na kusisitiza suala La Amani ambalo ndiyo msingi Mkubwa katika
kuabudu.
Naye mchungaji wa kanisa hilo
la KKKT Mchungaji Prosper Kinyaha amemuombea maombi maalum mkurugenzi
Kihamia Mungu aendelee kumbariki kwa moyo wake wa ushirikiano na upendo
wa kuchangia michango hiyo kwa kushirikana na wadau aliokuja nao.
Katika
hafla hiyo mkurugenzi Kihamia alikutana na walimu wake waliomfundisha
katika shule ya sekondari magamba Boys iliyoko wilayani Lushoto kwa
kipindi 1986 mpaka 1992 ambapo wameshangaa kumuona mwanafunzi wao ambaye
kwasasa ni kiongozi wa jiji la arusha na kusema kuwa alikuwa ni moja ya
mwanafunzi msikivu kwa walimu wake.
EmoticonEmoticon