Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana kuanzishwa kwake kulianzia katika zahanati.
Hayo
ameyasema na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara katika Hospitali
ya Wilaya ya Mkuranga, amesema Hospitali ya Mkuranga kuanzia majengo
kuwa mbalimbali tofauti na inavyotakiwa.
Amesema
katika ziara hiyo amesema hata mfumo wa kuhifadhi taka katika hospitali
hiyo hauko sawa pamoja na hali ya usafi katika wodi ya wazazi.
Dk.Kigwangala
amesema kutokana na mazingira yaliyopo katika hospitali itachukua hatua
katika kuiweka hospitali hiyo kwenye .ubora mzuri.
Aidha
amesema Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amekuwa bega kwa bega na
hospitali ya Mkuranga ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau katika
kusaidia hospitali katika maeneo mbalimbali.
Dk.
Kigwangala amesema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali kujitoa katika
kufanya masuala mengine bila kusubiri serikali kuu ikiwa ni pamoja na
kutenga siku ya kufanaya usafi katika hospitali hiyo.
Nae
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega amesema ziara ya Naibu Waziri huyo
itazaa matunda kwa hospitali ya Mkuranga kuwa na sifa ya hospitali ya
Wilaya.
Amesema
watakuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwa mara moja kwa wiki hali
ambayo inaweza kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamis
Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
na Halmashauri wakati ziara yake katika Hospitali hiyo. .(picha zote na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza na watendaji wa
Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri katika ziara ya Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangala.
Mbunge
wa Mkuranga, Abdallah Ulega akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangala kufanya ziara katika hospitali hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangala akikabidhi gari la wagonjwa na vifaa kwa Uongozi wa Wilaya
ya Mkuranga
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangala akitembelea na kukagua wodi mbalimbali katika Hospitali ya
Wilaya ya Mkuranga katika ziara yake aliyofanya katika Hospitali hiyo.
(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa katika Hospitali ya Mkuranga.
EmoticonEmoticon