BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

May 26, 2017
NGEN1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipongezwa na baadhi ya Watendaji wa Wizara baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN3
Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi na viongozi wakuu wa Wizara; Naibu wake; Angeline Mabula, Katibu Mkuu; Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu; Dkt. Moses Kusiluka wakijadili jambo nje ya ukumbi wa bunge, baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN4
Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi wakifurahia na watendaji wa Wizara na Taasisi baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN5
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini; Edwin Ngonyani akipata elimu ya matumizi ya vifaa vya upimaji Ardhi vya kampuni ya Surveying Equipment Service Centre (EA) LTD/ SESC (EA) LTD katika eneo la bunge baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
…………………………………………………
Waziri Lukuvi aahidi kasi ya Upimaji Nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi aahidi ongezeko la Upimaji wa Ardhi Nchini baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara – Bungeni.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kupatikana kwa vifaa zaidi vya upimaji, baada ya hoja za wabunge; Mhe. Lukuvi amesema Wizara imejipanga kutoa mafunzo kwa wapima wa Ardhi nchini na hivyo kasi ya upimaji itaongezeka nchini kwani vifaa hivyo vya aina ya RTK vina uwezo wa kupima ekari elfu 30 kwa wakati mmoja. Alisema, vifaa hivyo vitatolewa kwa Halmashauri nchini bila gharama. Aliongeza kuwa Serikali itanufaika kwa kupata ongezeko la mapato ya Kodi ya Pango la Ardhi zaidi.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali iliahidi kuidhinisha ramani za Upimaji zenye viwanja 200,000 na mashamba 400. Hadi kufikia 15 Mei, 2017; ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 118,502 na mashamba 374 ziliidhinishwa. Katika mwaka wa fedha 2017/18 Wizara itaidhinisha ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 200,000 na mashamba 400.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »