WIZARA TATU KUSHIRIKIANA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU

May 27, 2017
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo akizungumza wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa kilichofanyika mjini hap
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo akielekeza jambo wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa kilichofanyika mjini
hap
 baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa.
 Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akiuliza swali kwenye kikao hicho
Picha ya pamoja
WIZARA tatu zinatarajiwa kushirikiana ili kuweza kukabiliana na wimbi la uvuvi haramu ambalo limekuwa tishio kubwa kwenye ukanda wa bahari ya hindi na maziwa hapa nchini  inayotishia usalama wa rasilimali zilizopo.
Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za baharibzinatunza na kulindwa.

Wizara ambazo zitashirikiana ni za Maliasili na Utalii,Nishati na
Madini,Sheria na Katiba na Ofisi ya Rais kutokomeza suala hilo kwenye maeneo ya bahari na maziwa.

Alisema kupitia mpango huo wanaweza kufanikiwa kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekuwa vikifanyika kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na kusababisha uharibifu wa mazalia ya samaki lakini pia kuleta madhara kwa viumbe.

Fatuma ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi upande wa wa Idara ya
Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
anayeshughulikia masuala ya uendelezaji wa rasilimali za uvuvi
 
Aidha alisema anaamini kupitia kikao hicho madiwani wanaweza kutumia elimu walioipata kuifikisha kwa wananchi hao juu ya athari za uvuvi haramu ili kusaidia kupunguza wimbi la tatizo hilo hasa kwenye maeneo ya ukanda wa bahari ya hindi kwani wao ndio wanajua mabomu yanapigwa kwenye maeneo gani.
 
“Ninaamini kikao hiki kitakuwa mwanga mzuri kwenu nyingi kuona namna ya kusaidia harakati hizi za kupambana na suala la uvuvi haramu kwani limekuwa na athari kubwa lakini sisi kama wizara hivi sasa tunashirikiana na wizara nyengine kwa lengo la kuzibiti suala hilo“Alisema Fatuma.

Akizungumzia suala la wavuvi wan chi jirani kuingia kuvua hapa nchini alisema ni kosa la kisheria kwani sheria hairuhusu wao kuingia na kuacha kufanya shughuli za namna hiyo kwenye maeneo yetu hivyo wanapaswa kuacha kujihusisha na jambo hilo.
 
“Sheria haiwahurusu wavuvi kutoka nchi jirani kuvua kwenye nchi
nyengine zilizopo jirani bila kuwa na idhini ya mamlaka husika hivyo niwatake wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja “Alisema.
 
Akizungumza kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu alisema anaamini kupitia elimu hiyo itawasaidia kushirikiana na kamati za BMU kupambana na uvuvi haramu.
 
“Nisema tunashukuru elimu hii ambayo ni muhimu kwa kutunza na
kuvilinda viumbe vya baharini hivyo tutashirikiana na kamati za BMU kuona namna ya kukabiliana na suala hilo “Alisema Naibu Meya huyo.

 Naye Mratibu wa Mradi wa Swiofish katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Nkana Mwagala alitoa wito kwa jamii kutunza rasilimali za bahari kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
 
Alisema kupitia kikao hicho wanaamini madiwani watakaa na wananchi hao ili kuweza kuwaelimisha madhara ya kufanya uvuvi haramu ikiwemo kuachana na suala hilo .

“Kwa sababu madiwani wanakundi kubwa la wananchi kwenye maeneo yao hivyo kupitia kikao hiki wanaweza kusaidia kuipa jamii uelewa kuhusu athari za uvuvi haramu lakini pia waweze mabalozi wazuri kuzilinda rasilimali za bahari kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho “Alisema.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »