Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisalimiana na Ally Khamisi Mvugalo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi. Leo Mei 25, 2017
Moja ya Majengo yaliyochakaa Shule ya Msingi Kawawa Iliyopo katika Kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema akizungumza kabla ya kumkaribisha MKuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori kuzungumza na wazazi na walimu wa Shule ya Msingi Kawawa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Ndg Badi Ahmed Darusi akisoma Taarifa ya shule ya Msingi Kawawa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 25, 2017 amefanya ziara ya kutembelea Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam.
Ziara hiyo ilikuwa na dhamira ya kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo hususani changamoto ya Upungufu wa Madarasa na Vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.
Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Mabibo, Mtendaji Kata ya Mabibo, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa, Uongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Shule, Walimu sambamba na Wazazi.
Katika ziara hiyo Mhe Makori amefikia uamuzi wa kuchangia Shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule kutokana na ubovu wa vyoo vilivyopo huku akiwasihi wananchi kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo.
Aidha ameahidi kuanzisha Harambee mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa kwani yaliyopo ni Madarasa 22 Kati ya Madarasa 68 hivyo kuna upungufu wa madarasa 46.
Kwa upande wa Matundu ya vyoo alisema kuwa upungufu ni mkubwa kwani yanahitajika matundu 136 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 26 pekee hivyo kuna upungufu wa matundu 110.
Mhe Makori amewasihi wazazi kushirikiana na walimu kufuatilia taarifa za wanafunzi kwani kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa wanafunzi hivyo kuifanya shule hiyo kuwa na ufaulu wa kiwango kikubwa.
Katika ziara hiyo Mara baada ya Mkuu wa Wilaya kuchangia Shilingi Milioni moja pia Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema alichangia mifuko nane ya Saruji, Kamati ya Shule Mifuko 10 ya saruji huku Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mabibo ukichangia jumla ya shilingi 200,000.
Mhe Makori alisema kuwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiandikisha kujiunga na darasa la kwanza kutokana na serikali kuwapunguzia wazazi jukumu la kulipa ada.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kufanya ziara katika shule hiyo Jambo ambalo limeibua hisia za mwanzo wa ujenzi wa madarasa sambamba na ujenzi wa vyoo vya kisasa.
Sawia na hilo pia amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na Mkuu wa Wilaya jambo ambalo anasema kuwa litapelekea kuwa na Maendeleo katika Wilaya ya Ubungo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Ndg Badi Ahmed Darusi akisoma Taarifa ya shule alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na Uhaba wa Samani, Upungufu wa walimu sawia na ukosefu wa fedha kwa ajili ya malipo ya Mlinzi.
Shule ya Msingi Kawawa ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Uwanjani ilianzishwa rasmi Januari 7, 1978 ambapo ilianza na madarasa mawili na ilijengwa kwa miti ikiwa na wanafunzi 60.
Shule hiyo inafanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwani kwa Takwimu za tangu mwaka 2012 Hadi 2016 haijawahi kushuka katika ufaulu chini ya asilimia 73.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
EmoticonEmoticon