Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko
Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana na Mstahiki
Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara
yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt.
Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es
Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI)
George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea
Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George
Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika
Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko
Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika
la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo akielezea jambo mbele
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya
Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo
la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la
Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wakifuatilia
maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa
ziara ya kikazi katika Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la
Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko
la Kariakoo Hetson Msalale Kipsi akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika
hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa
ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika
la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Meneja Mkuu wa Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC), Rwandiko Manumbu akiwasilisha
taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene
(kulia) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko
Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC)
leo.Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni akipokelewa na baadhii ya wajumbe wa Bodi za Mashirika ya
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) NA Shirika la Masoko Kariako
alipowasili katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la
Kariakoo Shimoni wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko
Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni(mwenye suti nyeusi) kuelekea katika Ofisi za Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara ya kikazi
kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama
Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi za Shirika la Maendeleo la
Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo
pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote: Frank Shija – MAELEZO
………………….
Nuru Juma – MAELEZO.
Serikali imeipongeza Bodi na
Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC)
kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto
wanazo kumbana nazo.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR
–TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika
la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko
Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.
Waziri Simbachawene alisema kuwa
amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi
kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya
mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.
“Pamoja na kuipongeza bodi hii
lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama
kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo
la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto
wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na
kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.
Simbachawene alitumia nafasi hiyo
kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo
la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine
itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.
Aidha ameutaka uongozi wa Shirika
la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa kuanzisha masoko sehemu mbalimbali
za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma kwa
wananchi na njia ya kuongeza ajira kwa vijana.
Alilitaka Shirika hilo kuachana na
mawazo ya kizamani na badala yake wajipange kimkakati ili kuendana na
wakati ikiwemo kufikiria namna ya kuwaza kushusha mizigo katika soko
hilo kwani serikali haitaweza kuruhusu maroli ya mizigo kufika katika
soko hilo ili kupunguza ya kuepuka msongamano katikati ya jiji.
Aliushauri uongozi huo uandae
mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha juu (Super Market)
na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana na bei halisi ya
soko kama ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa wakitoza ili kukuza
kipato kwa Taifa.
Waziri Simbachawene ameahidi
kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua changamoto ambazo
zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii kwani
Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na kuchapa kazi.
Awali akiwasilisha taarifa fupi ya
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Shirika
hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokumbana
nazo Shirika limefanikiwa kutoa shilingi milioni 140/- kama gawio kwa
mwanahisa wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
“Mhe. Waziri, kwa mara ya kwanza
tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza kutoa gawio la kiasi cha
shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji na haya ni mafanikio
makubwa kwetu,” alisema Manumbu.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa
Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amempongeza Waziri Simbachawene kwa
utayari wake wa kushughulikia changamoto zinazo yakabli mashirika hayo
ikiwa ni pamoja na kutenga muda wake kuja kusikiliza matatizo yao.
Pamoja na pongezi hizo Mwita
alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) kuangalia
uwezekano wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyokuwa amedhamiria wakati wa
uanzishwaji wa Shirika hili.
Shirika la Maendeleo la Jiji la
Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo ni mashirika ya Umma
yanayoongozwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
chini ya Sheria za Makampuni namba 2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge
namba 36 ya mwaka 1974, “The Kariakoo Market Corporation Act, 1974
EmoticonEmoticon