Meneja
wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, akiongea na wanafunzi wa shule
ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo katika semina ya
kuwajengea uwezo wa kujiamini na kukabiliana na changamoto mbalimbali
chini ya mpango unaojulikana kama HerAfrica.
Wanafunzi
wasichana wa shule ya sekondari ya Premier iliyopo Bagamoyo katika
picha ya pamoja wakati wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na
mpango wa HerAfrica.
—
Kampuni
ya TBL Group imeelezea dhamira yake ya kuunga mkono serikali na taasisi
mbalimbali zinazotekeleza mpango wa kuwajengea uwezo watoto wa kike na
kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na
kusababisha wabaki nyuma.
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Masuala yanayohusiana na kampuni wa TBL Group, Georgia
Mutagahywa,aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akieleza jinsi
kampuni ilivyoshiriki katika semina ya mpango wa kuzungumza na wasichana
kuhusiana kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ujulikanao
kama HerAfrica.
“Mtazamo
wetu ndani ya kampuni suala la jinsia tunalipa umuhimu mkubwa kwa kuwa
tunaamini kuwa wanawake wanao uwezo wa kufanya vizuri wakipata fursa na
kuondokana na changamoto zinazosababisha wabaki nyuma na tutaendelea
kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi mbalimbali zinazopambana na
usawa wa kijinsia na kuondokana na mila potofu zinakwamisha wanawake na
kusababisha wabaki nyuma” alisema Mutagahywa.
Katika
semina ya taasisi ya HerAfrica iliyofanyika katika sekondari ya
wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo, Meneja wa Mawasiliano wa TBL
Group, Zena Tenga ,aliungana na wanawake wengine kutoa mada za
kuwajengea uwezo wa kujiamini wasichana wanaosoma katika shule hiyo.
Mbali
na mada za kuwajengea uwezo wa kuamini pia wanafunzi hao wasichana
walielezwa changamoto mbalimbali wanazoweza kukutana nazo katika ujana
wao zinazoweza kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zao na walipewa mbinu
na mikakati ya kuzikabili ili waweze kutumiza ndoto zao pia walielezwa
umuhimu wa kujibidiisha na masomo yao kwa kuwa elimu ni silaha pekee
itakayoweza kuwakomboa.
Mratibu
wa programu hiyo nchini,Lilian Matari,kutoka kampuni ya Ushauri wa
kitaalamu ya LAS alisema kuwa hii ni semina ya pili ya kuongea na
wasichana kufanyika na mkakati wa kampuni ni kuendesha semina nyingi
nchini kote ili kuwafikia wasichana wengi hususani waliopo mashuleni.
EmoticonEmoticon