SERENGETI BOYS: NI KUJIPANGA UPYA
Safari
ya Serengeti Boys - timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17,
inaendelea licha ya jana Mei 21, mwaka huu kuondolewa kwenye hatua ya
makundi ya kuwania taji la Afrika hapa Port Gentil nchini Gabon.
Serengeti
Boys ilifungwa bao 1-0 na Niger katika mchezo uliofanyika , hivyo
kufanya matokeo ya timu zote mbili kufanana kwa pointi, idadi ya mabao
ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15,
mwaka huu.
Serengeti
Boys ilikuwa Kundi B pamoja na Mali iliyoongoza kundi hilo kwa
kufikisha pointi saba, ikifuatiwa na Niger yenye pointi nne sawa na
Tanzania pamoja na Angola iliyoambulia pointi moja.
Licha
ya Serengeti Boys kulingana na Niger, lakini wapinzani wa Tanzania
walipenya kwenda hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
faida ya ushindi katika mchezo ambao umekutanisha timu hizo.
Kanuni
hiyo ya mashindano ya CAF inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa
maana zinapokutana timu mbili zenye uwiano wa pointi na magoli
kinachoangaliwa hapo ni timu gani ilimfunga mwenzake walipokutana na
ndipo matokeao hujulikana,
Kwa
jana Mei 21, mwaka huu hali hiyo ilijitokeza hivyo Niger kusonga mbele
kwa kuwa aliifunga Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa
Prt Gentil nchini Gabon.
Akizungumzia
matokeo hayo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi amesema: “Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.”
Alizungumza
hayo kwa nyakati tofauti, Malinzi alisema: “Tujipange sasa kwa
yafuatayo: Michezo ya kufuzu (Qualifiers za 2019 Afcon U20 zinafanyika
mwakani kuanzia mwezi June. Vijana hawa watashiriki.
“AFCON
U17 finals (Fainali za AFCON za vijana wenye umri wa chini ya miaka 17)
zinafanyika Tanzania mwaka 2019,” amesema Malinzi na kuongeza:
“Serengeti Boys hii ya sasa inakuwa Ngorongoro Heroes (Vijana wa u20 na
ikishapumzika kwa muda, itaingia tena kambini.”
Amesema
kwamba vijana wa Tazania wenye umri wa chini ya miaka 15, walioko Shule
za Alliance Mwanza wanakuwa Serengeti Boys wapya.
“Hakuna
muda wa kusononeka ni kuchapa kazi tu. Kikubwa tunaandaa Taifa stars ya
kwenda World cup 2026 na qualifiers zake zitaanza mwaka 2024. Kwa sasa
timu inajiandaa kuingia kambini kwa ajili ya kuivaa Lesotho,” amesema.
Kocha
Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema timu yake imepoteza mchezo
huo kwa makosa ya kimchezo na bahati haikuangiwa kwa vijana wa Tanzania
katika mchezo dhidi ya Niger.
VPL: MCHEZAJI BORA WA MWEZI MEI NI MOHAMMED HUSSEIN
Mchezaji
wa timu ya Simba SC, Mohamed Hussein amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.
Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.
Katika
mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika
zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika
nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.
Kwa
kushinda tuzo hiyo, Kaseja atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania.
Wachezaji
wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba
(Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda
(Novemba).
Wengine
ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar
(Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera
Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).
MSUVA, MUSSA WAGAWANA KIATU CHA DHAHABU
Washambuliaji
Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka
wafungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017
iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.
Kutokana
na wachezaji hao kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga
mabao 14, watapata zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000 kwa
kila mmoja.
Yanga
imemaliza Ligi hiyo ikiwa bingwa kwa ponti 68 na kufunga jumla ya mabao
57, wakati Ruvu Shooting iliyomaliza katika nafasi ya saba kwa ponti 36
imepachika jumla ya mabao 28.
Watakabidhiwa
zawadi hiyo katika hafla ya tuzo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom msimu wa 2016/2017 itakayofanyika keshokutwa (Mei 24 mwaka huu)
kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon