Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetenga kiasi cha shilingi billioni mbili ili kukarabati miundombinu ya shule kongwe za Sekondari za kilakala na Mzumbe kwa wamu ya kwanza ikiwa ni kuboresha kiwango cha elimu na kurudisha umaarufu wa shule hizo ambazo zimetoa wasomi wakubwa na watalaamu mbalimbali hapa nchini.
Akiongea
katika makabidhiano ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu
ya shule kongwe ya Mzumbe sekondari na kilakala sekondari mkoani
morogoro Kaimu mkurugenzi mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean
Shirima amesema ukarabati wa shule hizo umeingia mkataba na mkandarasi
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya shillingi Billioni 2 kwa
awamu ya kwanza huku meneja waShirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi.
Veneranda Seif amehaidi kuhakikisha ujenzi wa miundo mbinu hiyo
unafanyika kwa kiwango kikubwa kuhakikisha thamani ya fedha iliyotolewa
inatumika kikamilifu.
Kwa
upande wake mshauri wa mradi, Bw. Thomas Kalugula amesema katika
upembuzi yakinifu kuna sehemu ya miundo mbinu inatakiwa kufanyiwa
ukarabati ikiwemo mifumo ya maji taka katika shule hizo huku wanafunzi
wakiipongeza mamlaka ya elimu Tanzania kwa kuwandalia mazingira bora ya
kujisomea.
Kaimu
Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima
(katikati) akimuelezea mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Sifuni Mshana
(kulia) kiasi cha fedha itakayotumika katika ujenzi wa awali wa
miundombinu ya shule mbili kongwe za kilakala na Mzumbe mkoani Morogoro
wakati wa ziara ya kukagua kiwango cha uchakavu wa miundo mbinu hiyo.
Mshauri
muelekezi wa Nousoto Associates, Bw. Thomas Kalugula akitoa taarifa ya
upembuzi yakinifu wa mahitaji ya ukarabati wa shule ya sekondari Mzumbe
mkoani Morogoro na kubainisha kuwa, ujenzi wa awali utahusisha mifumo ya
maji taka ambayo haifanyi kazi ipasavyo huku akihaidi kuwa watasimamia
ujenzi huo hadi hatua ya mwisho.
Meneja
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Morogoro, Bi. Veneranda Seif
akikabidhiwa mkataba wa ujenzi wa shule kongwe za Kilakala na Mzumbe
ambazo zilielezwa kugharimu kiasi cha shillingi billioni mbili katika
ujenzi wa awali huku mkataba huo ukimtaka mkandarasi huyo kuanza ujenzi
mapema 2 Juni mwaka huu.
Kaimu
Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu (TEA), Bi. Graceana Shirima akiwa na timu ya
wataalamu wakiwemo waandishi wa habari mkoani Morogoro katika kukagua
miundo mbinu ya shule ya sekondari Kilakala ili kujionea hali halisi ya
majengo na kubaini uwepo wa jengo ambalo halitumiki kutokana na kukosa
ukarabati.
Walimu
wa shule ya Mzumbe mkoani Morogoro na wakandarasi wakiwa na kaimu
Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima
wakiangalia shimo la maji taka ambalo lilielezwa kuwa limetitia
likazuiwa na magogo kwa tahadhari zaidi hata hivyo majani yanaoneka
yameota katika eneo hilo huku likisikika kutoa harufu kali ya vinyesi.
Kaimu
Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima
(katikati) akiwa darasani kukagua dali zilizotoboka katika moja ya jengo
la kujifunzia shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro.
Timu ya watalaamu wakiwa na mkandarasi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) mkoa wa Morogoro, Bi. Veneranda Seif (wa pili kutoka nyuma) katika
ziara ya Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi.
Gracean Shirima akikagua majengo yaliyochakaa.
Bweni la wanafunzi kama linavyoonekana.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Mwalimu Wencelaus Kihongoti akimpa
maelekezo machache Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe.
Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
EmoticonEmoticon