Katibu
Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H.
Bakari (katikati) akiongoza kikao cha pamoja na Benki ya Maendeleo ya
Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara
hiyo.
Mjumbe
wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo
(wapili kulia) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Biashara,
Viwanda na Masoko Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,
Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari.
Wajumbe
wa kutokana TADB wakifuatilia kwa makini mazungumzo na uongozi wa
Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Mazungumzo hayo
yalifanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kulia) akieleza
dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali katika
kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Mkurugenzi
wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati)
akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati
walipotembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Biashara,
Viwanda na Masoko Zanzibar (hawapo pichani). Wengine pichani ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Meneja wa
Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kushoto).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H.
Bakari akihiimiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao
Makuu ya Wizara hiyo.
Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Na Mwandishi wetu,
Wizara
ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar imesema itakuwa ya mwanzo
kuanza kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ili kuchagiza uwekezaji katika sekta ya
uchakataji wa mazao na masoko ili kuongeza tija kwa maendeleo visiwani
Zanzibar.
Mkakati
huo umewekwa bayana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bakari H. Bakari
wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake.
Bw.
Bakari amesema kuwa ujio wa Benki hiyo unatoa fursa kubwa sana kwa
sekta zilizo chini ya wizara yake ikiwamo biashara, viwanda na masoko.
“Tuna
imani kubwa ujio wa TADB utatusaidia kutatua changamoto zinazozikabili
sekta hizi ambazo zinakabili na changamoto ikiwemo ukosefu wa masoko ya
mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji;
maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu
vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya
kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo,” alisema.
Akizungumza
wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw.
Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali
kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya
kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji
wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha
mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye
sekta ya Kilimo.
Bw.
Assenga alisema visiwa vya Zanzibar vitaingizwa rasmi katika mpango wa
biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara wa
mazao ya kilimo visiwani humo kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
EmoticonEmoticon