Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima
akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa
shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa TEA.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela akizungumzia
faida zinazotokana na mradi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya
Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa
ufadhili wa Mamlaka ya Elimu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima
akimkabidhi mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar
es Salaam Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Miliki NHC Bw. Hassan Mohamed,
ukarabati huo unafanywa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima
akiwaongoza wadau walioshiriki hafla ya makabidhiano ya mkataba wa
ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa
na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukagua baadhi ya majengo na miundo
mbinu ya shule hiyo itakayofanyiwa ukarabati.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi akishukuru Mamlaka ya
Elimu Tanzania kwa kuamua kukarabati miundo mbinu ya Shule hiyo ili
kukuza kiwango cha elimu. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.
Msongela Palela
Baadhi
ya Majengo ya Shule ya Sekondari Pugu yatakayofanyiwa ukarabati na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) na yatagharimu zaidi ya milioni mia tisa. (Picha zote na
Frank Mvungi-Maelezo).
Na Fatma Salum- MAELEZO
Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA) imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa
kukarabati Shule ya Sekondari Pugu iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi mkataba wa ujenzi kwa Mkandarasi wa
mradi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima alieleza kuwa
zaidi ya shilingi milioni 984 zitatumika katika awamu ya kwanza ya
ukarabati wa shule hiyo.
“Awamu
ya kwanza ya ukarabati wa shule hii itaanza tarehe 1 Juni, 2017 na
itafanyika kwa muda wa miezi minne. Ukarabati katika awamu hii
utahusisha madarasa, vyoo kwa ajili ya wanafunzi walemavu, mabweni,
jengo la utawala, mifumo ya TEHAMA, mifumo ya maji safi na maji taka
pamoja na mifumo ya umeme”alifafanua Bibi. Shirima.
Alieleza
kuwa zoezi hilo la ukarabati lilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa
kubaini hali halisi ya mahitaji ya ukarabati na kazi hiyo ilifanywa na
Mtaalamu Elekezi (Consultant).
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela
Palela alipongeza jitihada za TEA za kukarabati miundombinu ya elimu
hasa kwa shule kongwe za Sekondari nchini kote mradi ambao utasaidia
kuboresha elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
“Manispaa
ya Ilala inaahidi kushirikiana na TEA na uongozi wa Sekondari ya Pugu
kutekeleza zoezi hili na kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi na ubora wa
hali ya juu.” alisema Palela.
Naye
Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi alieleza kuwa
shule hiyo ina historia kubwa katika nchi yetu na kuishukuru Serikali
kupitia TEA kwa ukarabati huo utakaosaidia kurudisha shule hiyo katika
hali yake ya awali.
Katika
mwaka wa fedha 2016/2017 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeazimia
kukarabati jumla ya shule kongwe za Sekondari 17 ikiwemo shule ya
Sekondari Pugu na zoezi hilo limeshaanza kwa shule za Sekondari Nganza,
Same na Ilboru.
EmoticonEmoticon