Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata
utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta
Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya
Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua
kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta
Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya
Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akipeana
Mikono na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James
Msuya mara baada ya uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star
Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja
wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha
moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akizungumza
mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya ukopaji wa Televisheni za Star
Times.
Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya akizungumzia namna ya kuapata mkopo kutoka benki hiyo
Sehemu ya Watumishi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Duka la Star Times Bamaga
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni
ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha
wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao
utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.
akizungumza
na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa
mpnago huo Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal,
amesema kuwa ubia huo unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia
rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa
awamu kupitia Benki ya TPB.
"wateja
wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es
salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo"
amesema Zuhra.
Akiongea
katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi amesema
ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya
Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na
jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya
kidigitali ya StarTimes.
Naye
Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo
imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano
ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja
kutumia.
“Najisikia
furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja
kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na
kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia
maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya
dunia”
Kwa
hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia
luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya
TPB.
Watanzania
waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali
kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.
Tunayo
matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu
kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh.
45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh
64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnwOdfqvwcOaT_nZcuM3FN8_EIfPZJF4JCcYxGDveC6Wb59-wlDWL-sMlGh7IXiYXYjBTY4Jkx9MEn-BH_1JoveRS8qnncdT1NExrpga2hcbBRbXXyYTGRsVgyQpD9si-i-T1GrxgX614/s640/_MG_0506.JPG)
Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi akizungumza na namna ya kutumia Luninga hiyo iliyo na king'amuzi ndani
Meneja Masoko wa Benki ya TPB,Amos Kisanga Akizungumza juu ya watu kufungua akaunti benki ya Posta na kuweza kukopa Luninga.
EmoticonEmoticon