KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja
na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikaochake cha tarehe 04 Mei,
2017imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge kuwa Mbunge wa VitiMaalum katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), kujazanafasiiliyoachwawazi na Mhe. Dkt. Elly Marco
Macha.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa
Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya
343,alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweponafasiwazi ya Mbunge wa
VitiMaalumkupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya
aliyekuwaMbunge wa VitiMaalumMhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na
hivyo kuwepo nafasi wazi.
Imetolewaleo tarehe 04 Mei, 2017 na:-
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
EmoticonEmoticon