Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa muda mfupi kabla ya
kufungua mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa
Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani
Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa
Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani
Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa
Makandarasi na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
…………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote
yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa
miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao
watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji
ndani ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati anafungua mkutano wa siku
Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.
Makamu wa Rais amesisitiza
wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja
na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia
ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio
vinginenevyo.
Makamu wa Rais amewataka
wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye
vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya
ujenzi wanayopewa.
Amesema kuwa Serikali itaendelea
kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu
zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali
ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za
kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya
Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima
Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”
Kuhusu madeni ya wakandarasi,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakandarasi kuwa
Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha
wakandarasi.
Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.
Kwa upande wake, Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa
Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili
kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora
unaotakiwa.
Waziri Profesa Mbarawa amekiri
kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo
hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi
hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa
kazi.
Amesema kuwa Wizara yake
itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili
waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.
Nae, Msajili wa Bodi ya
Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa
wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa
Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000
kote nchini.
Msajili huyo pia amesema kuwa
katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua
miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia
71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali
ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na
kutozingatia usalama wa wafanyakazi.
Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango
EmoticonEmoticon