Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza. Waziri Dkt.Mwakyembe alimwakilisha Rasi John Pombe Magufuli.
Dkt.Mwakyembe aliwaasa waandishi wa habari kuwa na weledi kwenye utendaji wao wa kazi ikiwemo kujikita kwenye habari za uchunguzi wa kina na siyo hisia alizosema atazilinda na kuzitetea huku akiwahimiza wahariri nchini kuwa na utaratibu wa kukutana na Mkurugenzi wa Habari Maelezo japo mara moja kwa mwezi ili kujadiliana kwa pamoja mafanikio na changamoto za utendaji kazi kwenye tasnia ya habari kwa manufaa ya taifa.
Aidha alionesha utayari wa kufungua milango ya majadiliano kuhusiana na sheria mpya ya vyombo vya habari nchini hususani katika baadhi ya vipengele vinavyolalamikiwa na wanahabari akisema sheria hiyo haijaandikwa kwenye mawe, ishara tosha kwamba kukiwa na mazungumzo, mabadiliko katika sheria hiyo yanaweza kufanyika.
BMGHabari
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza.
Kitomari alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya waandishi wa habari 100 kote duniani waliuawa mwaka 2016kutokana na majukumu yao ya kazi huku pia kukiwa na matukio ya upigwaji na utekaji wa waandishi wa habari ambapo kwa Tanzania zaidi ya kesi 30 za manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ziliripotiwa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fikra Makini, Nyakati za Changamoto, Jukumu la Vyombo vya Habari katika kudumisha Amani, Usawa na Jamii Jumuishi".
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi mkazi wa taasisi ya FES nchini Tanzania, Michael Schulteiss, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
EmoticonEmoticon