INUKA KUTOA ELIMU ZA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWA MIKOA MINNE NCHINI

March 11, 2017
Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania (INUKA) inatarajiwa kutumia kiasi cha milioni 20 kwa ajili ya kutoa elimu kwenye mikoa minne iliyopo hapa nchini lengo kubwa kuielimisha jamii juu ya madhara ya dawa ya kulevya ili waweze kubadilika na kuachana nayo.

Hatua ya Taasisi hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya kuhakikisha vita ya dawa za kulevya hapa nchini inakwisha ili vijana waweze kuepukana na matumizi hayo ambayo yanaathari kubwa kwa maendeleo ya uchumi wao na jamii
zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa  na Mratibu wa Inuka Kanda ya Ziwa, Gaudance Msuya wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani hapa ambapo alisema elimu hiyo itakuwa chachu ya kuibadili jamii kuachana na matumizi hayo ambayo yamekuwa na athari kubwa.

Alisema licha ya hivyo lakini pia itasaidia kuipa jamii uelewa ambao utawawezesha kupiga vita matumizi ya madawa hayo ambayo yameathiri nguvu kuvwa ya vijana kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aliitaja mikoa ambayo inatarajiwa kunufaika na elimu hiyo kuwa ni Tanga, Iringa, Ruvuma na Lindi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha vijana wanaondokana na matumizi ya dawa hizo.

“Tatizo la dawa kuvelya limekuwa kubwa sana kwenye jamii hivyo sisi kama Taasisi tumeona ni bora tuunge mkono kulitokomeza kwa kutoa elimu kwa jamii na watumishi wa serikali “Alisema.

Aidha alisema lengo kubwa ni kuhakikisha jamii inaelimisha kuhusu madhara ya matumizi hayo ili waweze kuachana nayo kama sio kwisha ili vijana waweze kuepuka kuyatumia.

“Lakini pia tunaomba makatibu tawala wa mikoa na wilaya tunapofika tushirikiane kwa pamoja kwenye vita hii kubwa ambayo inaathiri nguvu kazi za vijana wengi “Alisema.

 Hata hivyo alisema kupitia elimu hiyo inaweza kuwasaidia vijana kubadilika ikiwemo kuachana nayo pia kutumia muda mwingi kujikita kwenye shughuli za kimaendeleo badala ya kushinda vijiweni.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »