WANAWAKE WANACHAMA WA CHA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAWI LA MIEMBENI MANZESE WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUFANYA USAFI.

March 11, 2017




Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese,Fatuma Mohamed (kulia) akishirikiana na wanachama wa chama hicho kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mtaa wao kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA




 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese wakishirikiana na wafanyakazi wa hospitali ya Mtakatifu Monica kuweka taka kwenye sehemu ya kuwekea uchafu kama ishara ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.

 Wanachama wa UWT Tawi la Mtaa wa Miembeni Kata ya Manzese wakiwa ndani ya Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzesed Darajani kwa ajili ya kufanya usafi kama ishara ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

 Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi hilo la Miembeni Manzese,Hanifa Mkura,akiongoza wakinamama wanachama wa chama hicho kufagia katika mazingira ya jengo la Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzese Darajani.
 usafi ukiendelea...






 Picha ya pamoja wakinamama wa UWT Tawi la Manzese Miembeni na wafanyakazi wa Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzese Darajani baada ya kufanya usafi.




NA ELISA SHUNDA,DAR

WITO umetolewa kwa wanawake kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii inayowazunguka katika ufanyaji wa usafi katika mazingira wanayoishi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko na yanayosababishwa na mazingira ya uchafu ukiwemo ugonjwa wa Kipundupindu,kuhara na Malaria.


Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mtaa wa Miembeni lililopo Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam jana,Fatuma Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kufanya  usafi katika maeneo ya mtaa wao ikiwemo eneo la ofisi za chama za mtaa huo pamoja na Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo eneo la Manzese Darajani.


“Leo sisi wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) UWT tawi la Manzese Miembeni tumejitokeza kufanya usafi katika mitaa ya eneo letu hili la Miembeni,ofisi za chama chetu za tawi pamoja na Hospitali ya Mtakatifu Monica ili kuonyesha mfano na kuwahamasisha wakinamama wenzetu kufanya usafi kwa kujitolea wenyewe bila ya kushurutishwa ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi na milipuko kama ugonjwa wa kipundupindu,kuhara hata na Malaria yanayotokana na wadudu wanaozaliana sehemu za mitaro isiyotembea na takataka zinazokaa kwa muda mrefu hivyo tumejitolea leo kufanya usafi ili mtaa wetu uwe mfano wa kuigwa na mitaa mingine”Alisema Mohamed


Aidha Mohamed alisema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi wa mtaa wao na kata ya Manzese kwa ujumla kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka lakini pia ni wajibu kwa kila mtu kufanya usafi katika eneo lake pamoja na kutosahau siku ya juma la mwisho wa mwezi lililowekwa na Rais Dk.John Magufuli la kufanya usafi katika mazingira yao.


Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Tawi hilo,Hanifa Mkura alisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wananchi hata wakinamama wamekuwa wagumu wa kushiriki kufanya usafi katika mazingira yao kutokana na hali jinsi ilivyo kuwa ngumu wanakuwa wanajikita kufanya biashara zao ili wajipatie kipato lakini wao kama wakinamama watawashauri wapange siku katika wiki wafanye usafi kwenye mazingira yao yanayowazunguka.

Imeandaliwa na Mtandao wa WWW.ELISASHUNDA.BLOGSPOT.COM/0719976633
Elisa Shunda

Photographer-Raia Tanzania Newspaper



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »