MKUU WA MKOA WA MWANZA AONGOZA MAZISHI YA MZEE ANTON R. KAYOMBO

February 10, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akizungumza wakati wa mazishi
 Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo wakati wa uhai wake
 Rc Mongela akimpa pole Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimpa pole MD Kayombo


Na Mathias Canal, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi waliojitokeza kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu wa vitabu vitakatifu vya Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Ndg Eliud Mwaiteleke kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
 Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo

Rc Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya taswira ya fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika maelekezo mbalimbali ikiwemo ushauri katika serikali.

Mongela aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi wote kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.


 Dc Happi akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamini Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijijini Misasi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda alisema kuwa Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye atakumbukwa kwa kazi njema alizozifanya wakati wa uhai wake ikiwemo kuwa mlezi bora wa familia yake na hatimaye kupatikana kwa kiongozi bora na mwenye weledi katika utendaji kazi. 


Akizungumza kwa niaba ya kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is Impossible Bwana Steve Nyerere ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Ubungo Ndugu John Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake ambaye ni Mlezi wake tangu akiwa mdogo sambamba na kuwasihi wananchi kuendeleza mshikamano na kupendana.

 Rc Makonda akitoa salamu za pole kwa niaba ya Viongozi wengine alioambatana nao kutoka Jijini Dar es salaam

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa salamu za shukrani akiwa na Mkewe

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.

Ameeleza kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.

 Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omaryakisaini kitabu cga wageni

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »