Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Dkt. Aziz P. Mlima jana amepokea msaada wa vifaa vya kufanyia
mkutano kwa njia ya video (Video Conference Facilities) kutoka Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme –
UNDP).
Baada
ya kupokea msaada huo, Balozi Mlima aliishukuru UNDP kwa msaada huo
ambao alieleza kuwa utasaidia shughuli za Wizara katika ofisi mpya ya
Wizara mjini Dodoma. Alisema msaada huo ni wa pili kwa Wizara katika
muda mfupi ambapo awali UNDP ilitoa ngamizi, printers na cameras.
“Tunamshukuru
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ambaye
ndio alianzisha suala hili na kuongea nanyi na kulisimamia bila kuchoka
hadi leo vifaa vinapatikana” “Kwa kweli ni mtu ambaye wakati wote
anapenda mambo anayoyasimamia yanatokea” Katibu Mkuu alimwambia
Mkurugenzi wa UNDP nchini Tanzania, Bi. Awa Dabo.
Kwa
upande wake Bi. Dabo baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa
mazungumzo kuhusu maombi ya msaada huo yalianza tokea mwaka 2014 lakini
kwa uwezo wa mungu vifaa hivyo leo vimekabidhiwa rasmi Wizarani.
Alielezea matumani yake kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa
utendaji kazi wa Wizara na pia utaboresha na kuimarisha zaidi uhusiano
na ushirikiano kati ya Serikali na UNDP.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 09 Februari 2017.
|
EmoticonEmoticon