LADY IN RED 2017 KUTIKISA JIJI LA DAR, NDANI YA KING SOLOMONI HALL JUMAMOSI HII!

February 10, 2017


Ni siku chache tu! zimesalia kuikamata Tarehe 11 mwizi huu 2017, kumbuka siku hiyo  ni siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tz, coz wanategemea kukutatishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani  hapa naizungumzia “Lady In Red”. 

Muandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, akizungmza na wabahabari Jana Tarehe 8/2/2017 huku akiwa ameambatana na wanamitindo wengine amesema kuwa, 
“Kwanza Show hii ni yakipekee pia inafaida kubwa sana kwa upcoming Designers, Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuweza kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu 11/2/2017 mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”. 

 Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnaombwa kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi Asante.
Wanamitindo wakiwa kwenye Press ya Lady In Red 2017





Asya Idarous

Picha ya pamoja ya wanamitindo baada ya Press ya Lady In Red 2017








Share this

Related Posts

Previous
Next Post »