TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

January 28, 2017
SOUPO
  • MTU MMOJA JAMBAZI APIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUTOROKA POLISI WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TARHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 00:30HRS USIKU KATIKA MTAA WA BWIRU KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA JAMBAZI ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA MAARUFU LA MUNGIKI, MWANAMUME, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 30 HADI 35, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUTOROAKA POLISI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA SILAHA AINA YA BASTOLA YENYE NAMBA ZA USAJILI TZCAR 97076 AMBAYO ALIIPORA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA  MWAKA 2013 MKOANI TABORA.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA YUPO KIJANA  ANAYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA MUNGIKI ANAYEMILIKI SILAHA, PIA ANAJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA HAPA JIJINI MWANZA NA KATIKA MIKOA YA JIRANI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA KUFANIKI KUMKAMATA MTUHIMIWA TAREHE 26.01.2017 MAENEO YA GREENVIEW KATA YA NYAMANORO WILAYANI ILEMELA. AIDHA MTUHUMIWA ALIPOHOJIWA NA ASKARI ALIKIRI KUWA NI KWEILI ANAMILIKI BUNDUKI AINA YA BASTOLA AMBAYO AMEIFICHA MAENEO YA SONGAMBELE KATIKA MLIMA WA KABOHORO KWENYE MAPANGO YA MAWE, MTUHUMIWA ALIWAONGOZA ASKARI  HADI ENEO ALIPOLIFICHA BUNDUKI HIYO NA KUIKUTA BUNDUKI AINA YA BASTOLA YENYE NAMBA ZA USAJILI TZCAR 97076 AMBAYO ALIKUWA AMEIFICHA KWENYE PANGO LA JIWE.
MTUHUMIWA ALIPOENDELEA KUHOJIWA NA ASKARI ALIDAI KUWA BUNDUKI HIYO ALIPEWA NA MTU MMOJA JINA TUNALIHIFADHI KWASABAU ZA KIUCHUNGUZI  ANAYEISHI MAENEO YA MEDICAL RESEARCH BWIRU, AMBAYE WALIKUWA WAKISHIRIKIANA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA UNYANG’ANYI  WA KUTUMIA SILAHA HAPA JIJINI MWANZA NA MIKOA YA JIRANI, AMBAPO  ALIKIRI KUWA AKISHIRIKIANA NA MWENZAKE HUYO WALIVAMIA MADUKA MAWILI YA MIHAMALA YA FEDHA (M-PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY) KATIKA MAENEO YA KILIMAHEWA KWA MSUKA AMBAPO   WALIPORA VITU MBALIMBALI KWA KUTUMIA SILAHA HIYO, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE NAMBA MZN/IR/632/2017 YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
ASKARI WALIONGOZANA NA MTUHUMIWA HADI ENEO HILO LA MEDICA RESEACH AMBAPO ALIDAI KUWA MWENZAKE  ANAPATIKANA  ILI AWEZE KUKAMATWA. AIDHA WAKATI WAMEFIKA ENEO HILO GHAFLA MTUHUMIWA MUNGIKI ALIKURUPUKA AKIWA NA PINGU MKONONI NA KUANZA KUKIMBIA UPANDE WA PILI WA BARABARA AMBAKO KUNAMSITU MKUBWA WA MEDICAL RESEARCH KWA LENGO LA KUTOROKA, ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI WAKIMUAMURU ASIMAME LAKINI ALIKAIDI, NDIPO ASKARI WALIMFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI, LAKINI NYINGINE KWA BAHATI MBAYA ZILIMPATA SEHEMU YA JUU YA KIUNO AMBAPO MTUHUMIWA ALIFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIKIMBIZWA HOSPITALI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.
AIDHA UCHUNGUZI UMEFANYIKA NA KUBAINI KUWA SILAHA HIYO AINA YA BASTOLA ILIYOSAJILIWA NA NAMBA  TZCAR 97076, MMILIKI WAKE NI BWANA JULIAN THADEUS LYIMO MIAKA 40, MENEJA WA MAMLAKA YA TUMBAKU TABORA NA MKAZI WA NYASUBI WILAYA YA KAHAMA MKOA WA SHINYANGA, AMBAYE ANAMILIKI SILAHA HIYO TANGU MWAKA 2011. AIDHA SILAHA HIYO ILIPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KATIKA BARABARA YA SIKONGE TABORA MWAKA 2013, NA KUFUNGULIWA KESI YENYE NAMBA TBR/RB/8345/2013.
KATIKA TUKIO HILO MAJAMBAZI WALIZUIA MAGARI KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO BARABARANI NA KUFANIKIWA KUPORA FEDHA NA VITU MBALIMBALI VYA ABIRIA AMBAPO BWANA JULIAN LYIMO AKIWA MMOJA WAPO ALIPORWA BUNDUKI YAKE AINA YA BASTOLA, KOMPYUTA MPAKATO AINA YA DELL, MIWANI YA MACHO PEA MBILI NA FEDHA KIASI CHA TSH 67,000/=.
ASKARI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA MISAKO YA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOKUWA WAKISHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA KUFANYA UHALIFU HAPA JIJINI MWANZA NA MIKOA YA JIRANI, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI WAHALIFU WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, LAKINI PIA ANAWATAKA WANANCHI WOTE WAWAKANYE WATOTO WAO WASIJIHUSISHE NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA UHALIFU MWINGINE, ILI KUFANYA MKOA WETU WA MWANZA UWE SALAMA NA TULIVU ILI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI AMBAO WAKIWEKEZA WATALETA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »