Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama
anavyojulikana jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na
kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia
mradi wowote uko chini ya kiwango.
Dkt.
Nchimbi amesema msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua
ukifanya watendaji kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali
zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia ipasavyo
utekelezaji wa maelekezo hayo.
Ameongeza
kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa
kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona
serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi
mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye
kazi ipasavyo.
Dkt.
Nchimbi amesema viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya
halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya mali zao zinazohamishika na
zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao
zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.
“Mradi
wakati unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam
wanauangalia bila kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia
umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa
‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango tutahakikisha
fedha ya serikali inarudi”, amesema Dkt. Nchimbi.
Aidha
katika kikao hicho na watumishi wote wa halmashauri hiyo amewaagiza
wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuwaruhusu wanafunzi ambao
hawana sare kuanza masomo huku utaratibu wa kuwafuatilia wazazi watimize
majukumu yao ukiendelea.
“
Baada ya elimu kuanza kutolewa bure, changamoto nyingine iliyobakia kwa
baadhi ya wazazi ni uwezo wa kuwashonea watoto wao sare za shule, sasa
ninaagiza wakuu wa shule za sekondari na Msingi wote Wilayani hapa
kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata kama hawajavaa sare za
shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare tu”, ameagiza
Dkt. Nchimbi.
Awali
kabla ya kuzungumza na watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika
mashamba ya wakulima ili kujionea na kushiriki na wananchi shughuli za
kilimo hasa mashamba ya viazi katika kijiji cha Nkungi na mashamba ya
mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani humo.
Dkt.
Nchimbi akiwa katika shamba la mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha
Nkungi alipanda viazi na kuhamasisha wananchi wengine walime mazao
ambayo yanatumia maji kwa ufanisi kama vile viazi, mihogo, matama na
uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini ili kujihakikishia uwepo wa
chakula.
Amewataka
watendaji hasa wa kada za kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa
mazoea hasa kuandaa taarifa za makaratasi bali wawatembelee wakulima na
wafugaji katika maeneo wanayofanya shughuli zao ili waweze kutoa ushauri
kwa kupata picha halisi.“Sipendi kiongozi anayesema yupo karibu na
wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo hivyo ni vyema
kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”, amesema
Dkt. Nchimbi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika
shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama
katika ziara yake wilayani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi
lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi
Wilayani Mkalama.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe
katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.
EmoticonEmoticon