MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

January 25, 2017

Na Woinde Shizza,Arusha

Mfanya biashara maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance  Moshi
(30) amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi  inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesh mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa
yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya  .
Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa
mahakamani.

Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha . 

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february  6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.

Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »