Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia

January 24, 2017


Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
WATANZANIA waishio nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamoja na kuangalia namna ya kutekeleza kiu ya nchi ya viwanda kama ilivyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, mwenye suti nyeusi, akifurahia jambo ofisini kwa Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten, alipofika ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo hija ya mwaka huu wa 2017.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, hayupo pichani walipokutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuangalia fursa za kimaendeleo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mjini Jeddah, Saudi Arabia na Balozi wa Tanzania nchini hapa, H.E Hemedi Mgaza, alipofanya kikao na Watanzania waishio nchini hapa kama njia za kushirikiana na wadau hao kwa ajili ya kupeleka maendeleo ya uhakika nchini Tanzania na kuisimamia kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Akizungumzia juu ya fursa ya uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Mgaza alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa nafasi yake kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao. Alisema mbali na Watanzania hao kuwekeza kwao kama uwezo wanao, pia wanaweza kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa ajili ya kuchangia fursa hiyo ya watalii inayolipa duniani kote.
Kikao kinaendelea.

Kikao kinaendelea.
“Tukitoka hapa kila mmoja awe balozi shupavu wa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania ili pamoja na mambo mengine, tuwe tumechangia ukuzaji wa uchumi wetu kulingana na uwezo wetu kwa kupitia sekta nyeti ya utalii, ambapo pia kama sehemu ya serikali nilisikiliza maoni na ushauri wao ili tusonge mbele..

“Tuonyeshe mazuri ya nchi yetu pamoja na sisi wenyewe kushiriki katika fursa za kiuchumi kuliko kusubiri wengine wafanye wakati tunajua fika kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuiletea maendeleo nchi yetu,” alisema Balozi Mgaza.

Kabla ya kikao hicho na Watanzania, Balozi Mgaza pia alifanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo, H.E Mgaza alijadiliana na Dr. Benten masuala mbalimbali yanayohusu maandalizi ya ibada ya Hijja ya mwaka 2017 na fursa kwa mahujaji wa Tanzania.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »