Mechi za raundi ya tano ya mechi za Kombe la Shirikisho la Azam
2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), zitaendelea kesho Jamatano
Januari 25, 2017 kwa timu za Singida United na Kagera Sugar kucheza
kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za The Mighty Elephant ya
Songea na Mashujaa ya Kigoma katika mchezo utakaofanyika Uwanja Majimaji
mjini Songea.
Katika mchezo huo ambao uliahirishwa Jumatano iliyopita, mshindi wa
kesho ndiye atacheza na Majimaji katika tarehe mpya itakayotangazwa hapo
baadaye kama ilivyo kwa mechi kati ya African Lyon na Mshikamano.
Leo Jumanne Januari 24, mwaka huu kuna mechi kati ya Mtibwa Sugar na
Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya
Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa
kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na
Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Pia
Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani
Mtwara.
EmoticonEmoticon