Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (wa pili kushoto)
akifuatana na Makamo Mkuu wa Chuo Prof. Idriss Ahmada Rai pamoja na
Viongozi wengine katika Gwaride la maandamano wakati wa sherehe ya
mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi
ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Riziki Pembe Juma
Baadhi ya Wahadhiri na wanataaluma wakiwa katika Gwaride
la maandamano wakati wa sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo
hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini
Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"
Baadhi ya wanataaluma wakiwa katika Gwaride
la maandamano wakati wa sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo
hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini
Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (katikati)
akiwapungia mkono wananchi na wanataaluma alipowasili katika viwanja
vya kampasi ya Tunguu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"Mkoa wa Kusini Unguja leo katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho (wa pili kulia) Makamo Mkuu wa Chuo cha "SUZA"Prof. Idriss Ahmada Rai
Baadhi ya wanataaluma wakisimama wakati mgeni rasmi Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" alipowasili katika
viwanja vya kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja palipofanyika Mahfali ya kumi na mbili ya Chuo hicho leo ,ambapo Wahitimu mbali mbali walitunukiwa Vyeti,Stashahada na Shahada
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 21.1.2017
MKUU wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema
kuwa Serikali itahakikisha mikopo inatolewa kwa wanafunzi wanaostahiki na kwa fani
iliozipa kipaumbele huku akiwasisitiza wanafunzi kuepuka udanganyifu na
kuirejesha mikopo hiyo kwa taratibu zilizopo.
Dk. Shein aliyasema
hayo leo huko katika viwanja vya Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),kilichopo Tunguu katika Mahafali ya 12 ya
Chuo hicho.
Akitoa nasaha zake Dk.
Shein aliwataka wanafunzi kuendelea kuitumia vizuri mikopo inayotolewa na wawe
waadilifu, ili huduma hizo muhimu zinazotolewa ziwe endelevu na ziwe na manufaa
zaidi kwa maendeleo.
Pia, alisema kuwa Serikali
itaendelea kuhakikisha kuwa wanaopewa mikopo hiyo wanakidhi viwango
vilivyowekwa na kutumia fursa hiyo
kuwataka wafanyakazi wa sekta ya umma wanaotaka kusoma kuziomba taasisi zao
kuwasomesha na si Bodi ya Mikopo ya Zanzibar kwani huo ndio uamuzi wa Serikali.
“Nililazimika
kuingilia kati na kusimamisha kwa muda utoaji wa mikopo ili Serikali iweze
kujiridhisha na utaratibu uliopo ambao baadhi ya wananchi
wakiulalamikia”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein kwa
mara nyengine tena aliuhimiza uongozi wa Chuo Kikuu cha SUZA kuongeza juhudi
katika kufanya tafiti zinazolenga katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbali
mbali zilizopo.
Aliitaka SUZA
kuendelea kushirikiana na kushauriana na Taasisi ya “COSTECH” na Tume ya Mipango
katika masuala mbali mbali yanayohusu tafiti, matumizi mazuri ya matokeo ya
tafiti hizo pamoja na suala zima la kutafuta ufadhili kwa ajili ya kufanya
tafiti.
Dk. Shein alitumia
fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wataalamu Wazalendo walioitikia wito wake na
kutekeleza kwa vitendo kuendesha mafunzo ya PhD ya Kiswahili na kueleza kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba itaendeleza juhudi za kuwashirikisha
Wanadispora katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika sekta zote
za kiuchumi na kijamii.
Alisema kuwa juhudi za
Serikali katika kuimarisha kilimo nchini zinakwenda sambamba na kuimarisha
sekta ya uvuvi hivyo, Serikali ina lengo la kuanzisha taasisi inayofundisha
mafunzo ya uvuvi na taaluma ya bahari sambamba na Kampuni ya uvuvi, uvuvi wa
bahari kuu na viwanda vya samaki.
Pia, Dk. Shein alisema
kuwa Serikali inafanya jitihada ya kuwa na chuo kitakachotoa mafunzo ya unahodha
wa vyombo vya baharini pamoja na mafunzo ya ubaharia, kazi ambayo inapendwa
sana na vijana hapa nchini.
Alisema kuwa agizo la
Serikali la kuiunganisha SUZA na taasisi tatu za Elimu ya Juu hapa Zanzibar
lina umuhimu mkubwa katika kuimarisha utoaji wa mafunzo na kuongeza fursa kwa wahitimu wa taasisi zilizounganishwa kwa
kupata vyeti kutoka Chuo kinachotambulika zaidi duniani.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza
haja kwa Televisheni ya SUZA kushirikiana na ZBC Televisheni pamoja na Kituo
cha Kwarara alichokizindua hivi karibuni
na kubadilishana uzoefu na utaalamu ili wafikie malengo waliyoyakusudia. Pia,
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutunuku zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri.
Nae Makamu Mkuu wa
Chuo hiho cha (SUZA), Profesa Idrisa Rai, alisema kuwa wahitimu wa mwaka wa
masomo 2015/2016 katika ngazi mbali mbali za masomo ambapo wanafunzi 861
wamehitimu mwaka huu kwenye masomo 23 ikiwa ni ongezeko la wahitimu 170 na
ongezeko la masomo 8.
Alisema kuwa kati ya
wahitimu wa mwaka huu, 62 ni wahitimu kwa ngazi ya Cheti, 440 ngazi ya
Stashahada, 356 ngazi ya Shahada ambapo wahitimu 2 walitunukiwa Shahada za
Uzamili za Sayansi za Mazingira na
Shahada ya Sayansi ya Kemia.
Pia, alisema kuwa kwa
mara ya kwanza chuo hicho kina mhitimu mmoja wa Shahada ya Uzamivu ambae
amemaliza masomo yake mwaka huu, ambayo hiyo ni Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili
ambayo alitunukiwa na Dk. Shein hii leo.
Aidha, Profesa Rai
aliwataka wahitimu hao wasidumazwe na changamoto za ajira na wasikate tamaa,
wasichoke kusoma na kujisomea zaidi katika fani
ambazo wana hamu ya kuzifanyia kazi.
Profesa Rai alitoa pongezi
kwa wanafunzi wa kike na kusema kuwa mwaka huu wahitimu wanawake wamefanikiwa
vizuri zaidi kuliko wahitimu wa kiume, licha ya kuwa na wanafunzi wengi ni wa
kike chuoni hapo na matokeo yameonesha kuwa wanafunzi wa kike ni mahiri zaidi
kuliko wanaume.
Alisema, kwa
kushirikiana na Ubalozi wa Italia, wataanzisha masomo ya lugha ya Kitaliana
somo ambalo litaifanya SUZA kusomesha lugha 8 za kigeni.
Pia, kwa kushirikiana
na UNICEF wanatarajia kuanza masomo ya Elimu ya Awali katika ngazi ya Shahada
na kuanzisha masomo mapya ya Shahada ya Uuguzi na Shahada za Uzamivu za Elimu
na ile ya Usimamizi wa Maliasili na Tabianchi ambapo pia, wameanzisha taasisi
ya uvuvi na masomo ya bahari.
Aliongeza kuwa ujenzi
wa ukumbi maalum wa Chuo kwa ajili ya Mahafali unaoendelea vizuri na wanatarajia
Mahafali yajayo kufayika katika ukumbi huo huku akieleza kuwa mwaka ujao
wataanza ujenzi wa jengo kwa ajili ya Skuli ya Elimu hapo Tunguu na jengo kwa
ajili ya skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni huko Nkrumah kwa ufadhili wa
Serikali ya China.
Akisoma risala kwa
niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee alieleza mafanikio
yaliopatikana chuoni hapo na kuiomba
Serikali kuwa karibu na Chuo hicho hasa katika fani mpya inazoanzishwa.
Nae Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma alieleza mashirikiano yaliopo kati ya Wizara
yake na Chuo hicho na kupongeza mafanikio yaliopatikana.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi na Elimu walipotunukiwa shada yao na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika sherehe ya
mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi
ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira walipotunukiwa shada yao na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika sherehe ya
mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi
ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Baadhi ya Wahadhiri wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa na Kikundi cha Brass Band cha Polisi katika sherehe
ya mahfali ya kumi na mbili ya Chuo Kikuu cha Tifa cha Zanzibar SUZA
yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (katikati) pamoja
na Viongozi wengine wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika
sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo
katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Ikulu.
EmoticonEmoticon