Waziri
wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na
watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea
shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya
uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo
cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi
wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein
Mansour akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Waziri
Tizeba.
Mkutano ukiendelea.
Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kuhusu, Bioteknolojia ya kisasa katika sekta
ya kilimo nchini.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa mada kuhusu utafiti wa mahindi yanayohimili ukame.
Taarifa ikitolewa mbele ya Waziri Tizeba (kushoto)
Safari ya kuelekea shamba la jaribio la mbegu za mahindi ikiendelea. Katikati ni Waziri Tizeba.
Mkurugenzi
wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso (katikati),
akitoa ufafanuzi kuhusu shamba hilo la jaribio hilo.
Waziri
wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (kulia), akizungumza na
watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi
yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa
Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma
leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na
Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.
Dotto Mwaibale, Dodoma
SERIKALI
imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha
tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba wakati
alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia
ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa
Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.
"Binafsi
nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini
tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani
maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo"
alisema Tizeba.
Alisema
ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya
utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.
Alisema
mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini
wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu
hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.
"Tusisubiri
taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais
Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona
namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa
mkulima.
Alisema
kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya
kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.
Alisema
leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika
jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.
Akizugumzia
kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya wananchi kuhusu matumizi ya vyakula
vya GMO alisema mitazamo hiyo inachochewa na wanaharakati kwa faida zao
binafsi na kama wanaushahidi wa jambo hilo ni vizuri wakatoa ushahidi
huo hadharani badala ya kupotosha umma.
"Kama
mtu anaushahidi huo namuomba aniletee badala ya kuzungumza mitaani
kwani wenzetu wa nchi zingine wanatumia vyakula hivyo na kama vingekuwa
si sahihi wangewezaji kuvitumia" alihoji Tizeba.
Mkurugenzi
Mkuu wa Costech Dk.Hassan Mshinda alisema kazi kubwa ya Costech ni
kufadhili tafiti mbalimbali na kuhakikisha zinawafikia walengwa na
akaishukuru serikali kwa hatua iliyofikia ya kuona taratibu na kanuni
zilizopo jinsi zinavyorudisha nyuma maendeleo ya tafiti hizo za
uzalishaji wa mbegu ambazo zikipatikana kwa wingi bei yake itakuwa ndogo
tofauti na sasa na kumkomboa mkulima.
EmoticonEmoticon