DC MUHEZA ASHIRIKI JOGGING,AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO.

January 14, 2017

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akishiriki kwenye mazoezi ya Jogging leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza,Desderia Haule

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye mazoezi hayo kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kujenga afya.


 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki mazoezi ya kuruka ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza



 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye kukumbia ikiwa ni kufanya Jogging inayofanyika kila mwezi wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza, Desderia Haule wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu katika Jogging ambayo hufanyika kila Jumamosi ya kwanza ya  mwezi kwa ajili ya kuimarisha miili na kuwaweka fiti wa kwanza kulia ni Mwandishi wa Azam TV mkoani Tanga,Mariam Shedafa akishiriki mazoezi hayo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew mara baada ya kumalizika mazoezi hayo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Jogging hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatenga maeneo  ya viwanja vya michezo ili kuwezesha vijana kushiriki kwenye michezo jambo ambalo linaweza kuwasaidia kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha.

Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya mazoezi kila Juma mosi ya pili ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili ya watumishi na vijana ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanaweza kuwanyemelea.

Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo kunapunguza fursa kwa wananchi na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hata kuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu ya kujipatia ajira.

“Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa vijana wengi ambao asilimia kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wa maisha”Aliseam Hajat Tumbo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa kufanya mazoezi hasa kwa watumishi wa Serikali.
 
Alisema ili kuweza kukabiliana na magonjwa hayo yasiyoambukizwa kama ugonjwa wa Moyo,sukari na shindikizo la damu lazima kauli ya makamu wa Rais ya kuhamasisha kufanyike mazoezi nchi nzima itekelezwe kwa vitendo na si maneno.

“Laima tubadilike kwa kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa hayo ambayo yamekuwa pigo kwa wananchi na hasa watumishi wa Umma,inatulazimu tupambane kukabiliana na hali hiyo kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zetu”Alisema Dk Mathew.

Naye Katibu Tawala Wilaya hiyo Desderia Haule ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilya alisema zoezi hili litakuwa ni endelevu na Serikali itatenga maeneo ya kutosha ya viwanja kwa ajili mazoezi na kukuza vipaji vya vijana .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »