HALMASHAURI YAIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA SHULE YA MSINGI HAZINA MISION KWA KUTOKUWA NA VIWANGO VYA UANDIKISHAJI

January 14, 2017


Na Woinde Shizza,Arusha

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya
msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa mara baada ya uongozi wa shule
hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza  watumishi
wake pamoja na  mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika uandikishaji wa shule.

Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja mara baada  siku chache zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi na walimu  wa shule hiyo na hivyo kutakiwa
kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya maagizo hayo kwa muda waliopewa.

Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo kaimu afisa elimu  shule za msingi katika jiji la arusha Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya
marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.

Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao, kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja
na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.

"Kwa kuwa uongozi  wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mlioagizwa ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu
katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice

Wananchi wa eneo hilo akiwemo  Diwani wa kata ya baraa Elifasi Ndetika akizungumzia  uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo  alisema kuwa ni halali kabisa kwani walikuwa na malundano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu
lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea marekebisho yakawepo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »