MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku ametoa
pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi
kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya
Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika
kipindi hiki kigumu.
Ajali ya Jahazi ambayo
ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria 12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.
Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani
maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea
Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na
dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi na kuzama
Akizungumza na MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na
uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.
Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda
12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye
eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa
kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.
Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo
nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali
pema peponi.
“Ajali sio jambo
ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo
vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani
hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba
alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na
usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.
Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa
wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.
Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado
hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa
mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi
eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.
Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na
majeruhi 25.
Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko
watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na
kuendelea na matibabu mengine.
EmoticonEmoticon