Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla mapema jana Oktoba 27,2017
ameweza kutembelea eneo la pori tengefu la Loliondo lililopo Wilayani
Ngorongoro Mkoani Arusha na kujionea mambo mbalimbali juu ya mgogoro wa
muda mrefu maarufu Loliondo.
Waziri
Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea katika eneo hilo katika kushuhudia
kiini hicho cha mgogoro uliozidi zaidi ya miaka 20, ambapo anatarajia
kurejesha majibu kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais mara tu baada ya
kumaliza ziara yake hiyo pamoja na kukutana na watalaam wake wa Wizara.
Waziri
Dkt. Kigwangalla ameweza kuoneshwa eneo lenye mgogoro baina ya
mwekezaji pamoja na wananchi wa jamii ya wafugaji kwenye eneo hilo
sambamba na kufuatilia mipaka baina ya maeneo mbalimbali yanayozunguka
mipaka ya pori hilo tengefu pamoja na hifadhi ya Serengeti.
Awali
Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika mkutano wa wazi kwenye Mji wa Wasso
aliweza kusitisha operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori hilo
tengefu la Loliondo na huku akiagiza mifugo yote iliyoshikiriwa na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa
huru huku ile mingine iliyofunguliwa kesi kuendelea kushikiriwa mpaka
shahuri la msingi litakapotatuliwa.
Aidha,
Waziri Dkt. Kigwangalla amewataka wananchi hao jamii ya wafugaji katika
mgogoro huo kuacha mara moja kuingiza mifugo ndani ya hifadhi licha ya
kusitisha Operesheni iliyokuwa ikifanyika na kuwataka wakae meza moja ya
majadiriano kupata ufumbuzi.
Akiwa
ndani ya pori hilo pia alishuhudia kundi kubwa la wanyama mbalimbali
kwenye maeneo hayo ambapo imeelezwa awali hawakuwapo kutokana na
kukimbia mifugo iliyokuwa imeingizwa na wafugaji hao.
Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla akiwasili eneo la Loliondo kushuhudia kiini cha mgogoro huo
Dkt.Kigwangalla
akiwa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Elimu Mh.Ole Nasha wakati alipofika kukagua kiini cha mgogoro
huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akitazama wanyama eneo
lenye mgogoro ambalo ni pori tengefu la Loliondo ambalo awali lilikuwa
limevamiwa pamoja na mifugo ya wananchi.
Dkt. Kigwangalla akifuatilia ramani yenye kuonesha eneo la pori tengefu la Loliondo
Baadhi
ya wanyama walioonekana wakati Waziri Dkt.Kigwangalla alipotembelea
pori hilo ambapo awali wanyama hao walitoweka kutokana na kuingizwa
kwamifugo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka (kulia) pamoja na Mhifadhi Mkuu
wa Serengeti William Mwakilema wakati wakikagua maeneo hayo yenye
mgogoro huo wa Loliondo.
Dkt.Kigwangalla wakikatisha katika maeneo hayo ya Loliondo wakati akikagua maeneo yenye migogoro.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa
wananchi waliokuwa wakitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro huo wa
Loliondo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza na wananchi
jamii ya wafugaji (Hawapo pichaani) wakati alipotembelea eneo la
Loliondo ili kubaini kiini cha mgogoro huo.