Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Mazungumzo
kuhusina na suala la NIshati ya jua na Balozi wa Morocco Nchini Mhe.
Benryane Abdelilah (katikati) kushoto ni Msaidizi wa Balozi Bw. Mrabet
Yazane.
Katikati Balozi wa Morocco Nchini
Mhe. Benryane Abdelilah akimsalimia Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alipomtembelea Ofisini kwake,
Kulia ni Msaidi wa Balozi Bw. Mrabet Yazane.
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipena Mkono na Balozi
wa Morocco nchini Mhe. Benryane Abdelilah alipomtembelea ofisini kwake
Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Kulia msaidizi wa Balozi wa
Morocco Bw. . Mrabet Yazane akimsalimia Naibu Waziri Mpina, kulia kwake
ni Mhe Balozi . Benryane Abdelilah. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
……………
NA ; Evelyn Mkokoi Dar es Salaam
Serikali ya Morocco iko tayari
kushirikiana na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari
zitokanano na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza kati mradi mkubwa wa
Nishati ya jua.
Akizungumza na Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina Ofisini kwake
jijini Dar es Salaam leo, Balozi wa Serikali ya Kifame ya Morocco Mhe.
Benryane Abdelilah amesema kuwa, Morocco ipo tayari kuwekeza katika
mradi mkubwa wa nishati ya Jua yani Solar energy, ili kuweza kusaidiana
na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kipato katika sekta mbali mbali
pamoja na kupunguza uzalishaji wa gas joto.
Pamoja na hilo, Balozi Abdelilah
ameitaka idara, kuainisha maeneo ya vipau mbele kwa upande wa mazingira
na kusema kuwa, mradi huo mkubwa wa uzalishaji wa Nishati ya jua
utakaotekelezwa na kampuni kutoka Morocco ya Masen Campany Limited,
utasaidia kuongeza matumizi ya nishati mbadala, pamoja na kujenga
mahusiano mazuri baina ya nchi hizi mbili hasa katika sekta husika.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi
hya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alisema
kabla ya uwekezaji wa mradi mkubwa wa aina hiyo, inatakiwa kufanyika kwa
tathmini ya athari ya mazingira na kumuahaidi balozi kuwa watakapokuwa
tayari zoezi hilo litafanyika kwa haraka , kwani uwekezaji huo utasaidia
kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji
wa miti kwa matumizi ya nishati ya kupikia na mradi utawafikia wananchi
wengi walio mbali na gridi ya taifa.
“kutokana na kukauka kwa vyanzo
vingi vya maji kunakosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi,
mradi huu utakuwa mbadala wa tatizo hilo, huu ni mradi ambao
utatusaidia, Alisisitiza Mpina.”
Balozi wa Morocco Mhe. Benryane
Abdelilah alimtembelea Naibu Mpina Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini
Dar es Saalam ikiwa ni katika kufahamiana katika utendaji baada ya
kufunguliwa kwa Balozi hiyo Nchini.
EmoticonEmoticon