MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI

April 07, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
 Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi

Na Nasri Bakari, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi Msakuzi.

Makabidhiano ya madarasa hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili (62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi Manispaa ya Ubungo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.

"Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.

MD Kayombo amesema kuwa mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa alivyokabidhiwa.

Pia ameahidi kuweka tarazo katika vyumba viwili vya madarasa ya zamani ambapo pia ameahidi kutoa mifuko Hamsini ya Saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya walimu na kuahidi kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano.

"Fedha hizi za kununua mifuko ya Saruji nitatoa kwenye mshahara wangu hivyo namsihi Mheahimiwa Diwani wa eneo hili naye aweze kuchangia ujenzi huu" Alisema MD Kayombo
 "Tunakushukuru sana Mkurugenzi kwa jitihada ulizozionesha katika shule hii kwa kipindi kifupi kwa kutununulia eneo la shillingi Millioni 35 na kutujengea madarasa matatu mungu akubariki sana" Alisema Bi Shahiri.

Mkurugenzi Kayombo amewasihi walimu wa shule hiyo kujitahidi kutunza mali za serikali zikiwemo madarasa, madawati na samani nyingine.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »