WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya
Wilaya ya Kibaha lifanye maamuzi ya kupima ardhi haraka na kutenga
maeneo kwa ajili makazi na viwanda ili kujiandaa na uwekezaji mkubwa.
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza
na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani mara
baada ya kukagua kiwanda cha kutengeneza magari ya zimamoto na matrekta
cha Equator SUMA JKT Limited kilichopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha mkoani
Pwani.
“Jiji
la Dar es Salaam limejaa, na Kibaha mjini pia hawana ardhi ya kutosha
kwa kimbilio pekee hivi sasa ni Kibaha Vijijini. Baraza la Madiwani
fanyeni maamuzi, pimeni ardhi na mtenge maeneo ya makazi, viwanda na
taasisi za elimu ili mkipata wawekezaji iwe rahisi kuwapa maeneo,”
amesema.
Waziri
Mkuu amesema ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa mkombozi kwa taasisi
nyingi na halmashauri nyingi nchini kwani zilikuwa zinashindwa kumudu
bei ya kununua magari ya zimamoto. “Baadhi ya Halmashauri nyingi
zilikuwa zinanunua gari moja kwa sh. milioni 500 na hiki ni kiasi
kikubwa mno kwa hiyo kiwanda hiki kitakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi
na halmashauri zetu,” amesema.
Amesema
maeneo mengi nchini yanahitaji magari ya zimamoto lakini yalikuwa
yanashndwa kumudu bei za magari hayo. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni
viwanja vya ndege, bandari, taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kama vile
shule za sekondari za bweni, Majiji, miji mikuu, Manispaa na Halmashauri
za Wilaya.
Amesema
ameguswa kukuta kiwanda hicho pia kina uwezo wa kutengeneza matreka na
zana za kilimo (farm implements) kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni
wakulima na wanategemea jembe la mkono. “Kupitia kiwanda hiki, matrekta
mengi yataunganishwa na nina imani bei itakuwa ya chini ili wananchi
waweze kumudu.”
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Equator SUMA JKT Ltd, Eng. Robert Mangazini alimweleza
Waziri Mkuu kwamba asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanda hicho imekamilika na
kwamba hivi sasa wako kwenhye hatua ya kufunga mitambo. Hata hivyo,
alisema wanaisubiri iwasili kutoka India.
Alisema
kiwanda hicho kikikamilika kitaweza kuunganisha matrekta 3,000 kwa
mwaka na magari ya zimamoto 100 na kubainisha kuwa faida za kuunganisha
magari hayo hapa nchini ni kuwa na uwezo wa kuzalisha vipuri ndani ya
nchi.“Tukiweza
kuzalisha vipuri hapa nchini kwa asilimia 60, umiliki wa magari haya na
matrekta utakuwa ni wa Tanzania na siyo wa kampuni za nje tena. Pia
tutakuwa tumefaulu kuhamisha teknolojia kwa vijana wetu,” alisema.
Alisema hadi sasa vijana 60 wamekwishapatiwa mafunzo ona wako tayari kuanza kazi mara uzalishaji utakapoanza Machi, 2017.Kuhusu
teknolojia ya utengenezaji wa magari ya zimamoto, Eng. Mangazini
alisema kiwanda hicho ni cha pili kujengwa barani Afrika cha kwanza
kikiwa huko Bassa, Afrika Kusini.
Mapema,
akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, mwakilishi wa Equator SUMA JKT
Ltd. Kapteni Farijala Mkojera alisema kiwanda hicho kinamilikiwa kwa
pamoja na kampuni ya Equator Automech Ltd ambao wana hisa asimilia 70 na
SUMA JKT inamiliki asilimia 30 ya hisa za kiwanda hicho.
Akizungumzia
ujenzi wa kiwanda hicho, alisema hadi sasa wamekwishatumia sh. bilioni
1.5 na kwamba hadi ujenzi utakapokamilika, wanatajia kuwa wametumia sh.
bilioni mbili. “Ujenzi ukikamilika, tunatarajia kuajiri wafanyakazi 200
katika fani mbalimbali,” alisema.
Alisema
wakianza uzalishaji, mbali ya magari ya zimamoto na matrekta, wataweza
pia kuunganisha mabasi na zana za kilimo kama vile combine harvesters.
“Tutakuwa tumefanikiwa kuhamisha teknolojia kutoka Russia (magari za
zimamoto) na India na Poland (matrekta). Tuna uhakika wa soko hapa
nchini katika Jumuiaya za EAC na SADC,” alisema.
Waziri Mkuu amerejea Dodoma mchana huu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa
reli inayounganisha reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Still Group
cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. 
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa
Still Group kilichopo Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi mkoani Pwani
Novemba 19, 2016. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kianda cha kuunganisha magari ya
zimamoto na matrekta cha Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani
Novemba 19,2016(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
EmoticonEmoticon