Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI
imesema Uislamu sio ugaidi hivyo dini isihusishwe na ugaidi na wala
Uislamu usitumike kama ngao ya kufanya uhalifu bali ugaidi ni uhalifu na
atakaejihusisha na ugaidi ashughulikiwe kama wahalifu wengine .
Yameelezwa
jana na mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo, kwenye kongamano la
Kiislamu lililoandaliwa na Marakazi ya Al Azhar Sharif, Changombe ,Dar
Es Salaam, lililofanyika ukumbi wa ccm, mkoa wa Arusha, lililokuwa
likizungumzia athari za Fatua zinazohalalisha umwagaji wa damu
zilizohifadhiwa na kutyumbisha amani na utulivu.
Kwenye
hotuba hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Monduli, Iddy Kimanta,
amesema vipo vitendo vingi vinafanywa na baadhi ya watu kwa kisingizio
cha dini ya Kiislamu jambo ambalo sio sahihi hatakidogo kwa kuwa dini
inakataza kumwaga damu au kuua nafsi isiyo kuwa na hatia .
Akasema
wanaojihusisha na ugaidi watashughulikiwa kama magaidi na kamwe
wasihusishwe na uislamu kwa kuwa dini haina uhusiano wowote na
ugaidi.KUhusu elimu, Kimanta,amewataka wazazi kuhakikisha wanasomesha
watoto wao elimu zote mbili ya Dunia na Akhera, na hivyo kuwajenga
kwenye malezi yaliyo bora ambayo yana maadili ya uislamu.kwa kuwa
yatawawezesha kujiepusha kujiingiza kwenye uhalifu na ugaidi.
”Arusha
ni eneo lipo kwenye hatari zaidi kwa kuwa tunakaribiana na maeneo
ambayo kama kama vijana wasipopelekwa kwenye malezi yenye maadili
watatumika kwenye ugaidi ,mfano anakuja mtu anachukua vijanakwa madai
anawapeleka nje kusoma na mzazi hahoji mtoto wake anaenda kusoma kitu
gani ”alisema, kimanta.
AmeseKUhusu
matumizi ya mitandao, amesema ipo mitandao mingi lakini sio yote yenye
nia njema na Uislamu hivyo wazazi lazima wawe makini kwa kuwa mitandao
mingi inalenga kuvuruga na kuwagawa na hatimae ni kuporomoka kwa maadili
katika jamii.
Amesema
kibaya zaidi wazazi nao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao na
hivyokusahau majukumu yao ya malezi na mitandao ina nguvu kubwa kuliko
Quraan tukufu na hivyo sasa wazazi na watoto wanaishi kimtandao tandao
badala ya kusomesha watoto ili wapate elimu yenye manufaa.
Awali
Shekhe wa mkoa wa Arusha, Shaaban bin Jumaa, amesema hivi sasa kuna
vikundi vingi vimezuka ambavyo vinakuwa vikitoa Fatua(MATAMKO) juu ya
dini ambayo yanapotosha na kusababisha mitafaruku na migogoro .Amesema
Fatua inatakiwa kutolewa na kiongozi mwenye elimu kubwa aliyebobea
kwenye dini na sio hali ilivyo ambaposasa mtu yeyote ambae hana elimu
kubwa wala sio kiongozi anatoa fatua.
Amesema
kinachosababisha hayo kutokea ni kutokuheshimiana ambapo kila mmoja
sasa anataka madaraka wakatihana sifa hiyo hivyo kilichopo ni kila mmoja
kumheshimu mwingine aliyemzidi elimu ya dini na hivyofatua zittaondoka.
Amesema
elimu ndogo ndio inayopelekea watu kufanya vitendo vya ugaidi na
kusingizia dini wakidai ni jihadi jambo ambalo sio sahihi hata kidogo.
EmoticonEmoticon