Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda akitoa maelekezo wakati akikagua uharibifu wa mazingira
katika mtaa wa Maweni Mjimwema uliosababishwa na wachimba kokoto.
……………………………………………………………………..
(NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es
salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia
ufumbuzi.
Ziara hiyo imeanzia katika wilaya
ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani,
Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua
mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
Akiongea na viongozi hao wa
wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua
kero za wanachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika.
“Nataka wafanyakazi wafanyekazi
kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua 80% ya
wafanyakazi wa serikali hawafanyikazi, asilimia 80 ya watumishi wa umma
hawafanyikazi, niwapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki
ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara,” alisema Mkonda.
Pia Makonda alisema hataki kuona
wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa
changamoto zao wakati serikali ina wafanyakazi kuanzia ngazi ya
vitongoji.
Aidha mkuu huyo ataelekea mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo ataangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na wachimba kokoto.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda akiongozana na wakuu wa wilaya za Kigamboni na Temeke
pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikagua uharibifu wa mazingira
katika mtaa wa Maweni Mjimwema uliosababishwa na wachimba kokoto
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda akiakizungumza na viongozi mbalimbali wa wilaya ya
Kigamboni hawapo pichani wakati aliofanya ziara ya kikazi ya kukagua
miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim
Mgandilwa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya wialaya katika ziara ya
mkuu huyo wa mkoa katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali
Hapi kulia akiwa pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Mh. Paul makonda hayupo pichani alipokuwa akizungumza
nao siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es samaa Mh.
Paul Makonda akizindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,
Hashim Mgandilwa katikati wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya
maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
EmoticonEmoticon