Kamishna Jenerali wa Magereza –
CGP. John Casmir Minja(vazi la kiraia) akiwa ameongozana na Mkuu wa
Gereza Karanga, Moshi, ACP. Hassan Mkwiche (kushoto) pamoja na Kaimu
Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Karanga, ASP. Michael Minja(kulia)
alipotembelea Kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ajili ya
ujenzi wa Kiwanda kipya cha kisasa cha viatu leo Oktoba 14, 2016.
Wengine pichani ni Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza –
CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akiangalia eneo ambalo limetengwa
kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu .
Kamishna Jenerali wa Magereza –
CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa
Magereza Mkoa Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo(kulia) alipokagua moja
ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha
kutengeneza viatu.
Eneo litakalojengwa kiwanda kipya
cha kisasa cha kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi. Kiwanda hicho
kitakuwa cha ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa jamii wa PPF.
Kamishna Jenerali wa Magereza –
CGP. John Casmir Minja akiangalia kiatu aina ya buti ndefu
zinazotengenezwa kiwandani hapo kwa ajili ya Maafisa na Askari wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama kama inavyoonekana katika picha
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).