Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe:Antony Mtaka akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mapema
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Banda na kupatamaelezo Mbali mbali juu ya Shughuli mbali mbali zinazofanywa Jeshi laKujenga Taifa Kambi ya Msange
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipata Maelezo katika Banda la NHIF
Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa Msisitizo
Na Woinde Shizza wa Globu ya jamii
Katimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu (MNEC) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Antony Mtaka ofisini kwake Bariadi Mkoa wa Simiyu katika mazungumzo yao waligusia Nyanja mbali mbali za kuimarisha mfumo wa kuwawezesha vijana kumudu kujiajiri ikiwa ni kupunguza malalamiko ya kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana. Kaimu Katibu Mkuu amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa
kuitikia na kutekeleza kwa vitendo agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kutoa fursa kwa vijana kupata ajira.

Amesifu mpango mkakati na utekelezaji wake unaojulikana Wilaya mmoja kiwanda moja ni kampeni ambayo
imeanza kuonyesha matukio ambapo vijana wanaonekana kuanza kuchangamkia fursa hiyo ndani ya wilaya za mkoa wa Simiyu, ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa wengine kuiga mfano mzuri ulioaznishwa na Mkoa wa Simiyu ili kuendana kwa pamoja na kasi na lengo la Rais la HAPA KAZI ambapo kinadharia linahimiza maendeleo
endelevu nay a haraka katika sekta zote za kiuchumi na kijamii hususan kwa Vijana.

Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemueleza Kaimu katibu Mkuu Shaka
kuwa wamejipanga vizuri katika kubuni na kuendeleza mipango yao sio kwa
maneno bali kwa vitendo ili kuufanya mkoa huo kuwa kitovu
cha viwanda vidodogo na vya kati na viwanda vikubwa . Kwasasa Simiyu imeanzisha kiwanda cha maziwa Wilaya ya Meatu na kiwanda cha Wilaya ya Maswa
cha viwanda vidodogo na vya kati na viwanda vikubwa . Kwasasa Simiyu imeanzisha kiwanda cha maziwa Wilaya ya Meatu na kiwanda cha Wilaya ya Maswa
Wakati
huo Kaimu Katibu Mkuu ametembelea na kukagua mabanda ya Maonyesho
yaliyozinduliwa tarehe 7 mwezi huu ikiwa ni miongoni mwa shuhuli za wiki
ya Vijana kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba wilaya ya
Bariadi Mkoa wa Simiyu.Kaimu Katibu Mkuu ameridhishwa na muamko wa
vijana katika kuonyesha muamko wa kuitikia wito wa Serikali wa kuwekeza
katika miradi yao ya kijamii ili kumudu kujiari na kupunguza kilio cha
ukosefu wa ajira sambamba na kuwanusuru wasijiingize katika matendo
maovu.