Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa
kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda
kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni mkuu
wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo
yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Tasisi ya
Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe( katikati) akiimba
wimbo wa maadili wa ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa
mafunzo ya upelelezi yanayofanyika katika chuo cha polisi kidatu.
Mafunzo hayo kwa askari 100 yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akiingia katika ofisi
ya mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kuzindua mafunzo ya upelelezi kwa
askari polisi 100. Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na
Hanns Sidel.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akisalimiana na
wakufunzi wa chuo cha polisi kidatu alipokwenda kuzindua mafunzo ya
upelelezi.Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns
Sidel. (picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)
Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro mhe. Dkt Kebwe Stevin kabwe amesema Jeshi la polisi
Tanzania ni kioo kwa majeshi ya polisi yalipo Afrika mashariki na hata
afrika kwa ujumla kutokana na umahili wake wa kutoa mafunzo mbalimbali
ya uaskari kwa baadhi ya nchi zilizopo afrika mashariki .
Dkt
Kebwe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi miwili ya
upelelezi katika chuo cha Polisi kidatu yaliyofadhiliwa na Taasisi ya
Hanns Sidel kwa askari polisi 100 waliotoka katika mkoa wa kipolisi
kinondoni ambalo wamechaguliwa kwa ajili ya kutekeleza kwa weledi mpango
wa kuborewsha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa huo
wa kipolisi.
“Huwezi
kwenda kujifunza katika nchi ambayo haifanyi vizuri, na ndioo maana
nchi za jirani huja Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna Jeshi la
Polisi Tanzania linavyo weza kuimarisha usalama wa raia na mali zao”
alisema Dkt Kebwe.
Aliwataka
askari hao wanafunzi wa upelelezi kujifunza kwa makini ili kuboresha
umahiri walionao katika kufanikisha upelelezi ili kuweza kuleta
mabadiliko ya kivitendo katika mkoa wa kinondoni kama eneo la mfano na
hatimaye maboresho hayo yaweze kuenea na kutekelezwa katika mikoa yote
nchini hivyo kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Kwa
upande wake mkuu wa kitendo cha kusimamia mapango huo wa kuboresha
usalama wa jamii kutoka makao makuu ya Polisi Naibu kamishina wa Polisi (
DCP)Godluck Mongi alisema mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio
makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi
na hakuna kesi itakayocheleweshwa chini ya siku sitini kwa maana hiyo
ndani ya siku sitini upelelezi wa kesi inatakiwa iwe imeisha.
Aliongeza
kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 askari
wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo ili waweze kuandana na kasi
inayotakiwa katika mpango huo wa maboresho ya usalama wa jamii.
Naye
mwakilishi wa taasisi inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina
lisema kwamba, ufadhili wa mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100
kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya
Hanns Seidel kuunga mkono jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha
ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kupitia mpango wa kuboresha
usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi
kinondoni.
Aliongeza
kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100
inaendelea kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na
maendeleo duniani kote.
Kwa
upande wake mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi
( ACP) Andrea Mwang’onda aliwataka wanafunzi wanapata mafunzo hayo ya
upelelezi kuzingatia kile wanachofundishwa na kufuta maadili yote ya
uaskari wakati wote watakapokuwa katika mafunzo hayo.
EmoticonEmoticon