Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt
John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana
Paselepa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha
maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt
John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu
wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la
medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Septemba 30, 2016
Ndege vita zikipita angani
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba
30, 2016
Ndege vita zikipita angani
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba
30, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt
John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu
wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho
ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko
Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016.PICHA NA IKULU.
…………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016
amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ”Amphibious Landing”
lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha
kamandi zote tano za JWTZ ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya
Makao Makuu na Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa
bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita
yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo
lililotekwa.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na
Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote
wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini,
uhakika na weledi wa hali ya juu.
”Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli.
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na
Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na
kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na
kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia
itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja
na kuipongeza JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo
Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili
ya kulinda nchi.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi
Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi wa Jeshi hilo.
Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi wa Jeshi hilo.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine
wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein
Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi
wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli,
amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa
ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious
Landing,
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
EmoticonEmoticon