Msanii akicheza na Nyoka wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Igombe marathon |
28 Septemba 2016 Tabora, Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania ikishirikiana na kampuni ya Chief promotions imetangaza rasmi kwamba tarehe 02/10/216 kampuni ya Chief Promotions imendaa mbio za kila mwaka kwa jina la Tigo Igombe Marathon.
Bright Kisanga ambaye ni Meneja Mauzo kutoka Tigo mkoani Tabora, alielezea kwamba, “lengo kuu la mbio hizi ni kusaidia vijana wenye vipaji vya riadha kupitia mchezo huo kuwa ajira yao kamili na pili kuwatangaza kitaifa na kimataifa, na Tigo ndio mdhamini mkuu, ambapo tumedhamini mbio hizi kwa 50m/-”
Lakini mbio hizi za KM 21 kwa wote,KM 5 za kujifurahisha na Mita 10 kwa watoto,Mita 10 kwa kinamama vilevile hutumika kuamsha ari ya wanajamii kutatuwa changamoto zao haswa za kimaendeleo.
Akiongea na waandishi habari, Meneja Mkuu wa Chief Promotions, Amon Mkoga alisema, “Kwa mwaka huu kundi litakalofaidika ni wasichana wa mashuleni kwa kushirikiana na wafadhili wa mbio hizi tumeamua kutoa Pad kwa wanafunzi kwa ajili ya kujinga kipindi cha hedhi, kama tunavyofahamu ingawa kumekuwepo kwa juhudi mbalimbali za kuinua elimu lakini bado mtoto wakike ana vikwazo vingi kimojawapo kushindwa kuhudhuria shule kipindi cha hedhi hii itasaidia kwa kiasi fulani kufikia malengo hayo.
“Mwaka huu marafiki wa Igombe Marathon watatoa misaada mbalimbali katika Hospitali ya Kitete kwa nia ya kuwa pamoja na wanajamii haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo.” Alieleza Mkoga
Mbio hizi zitaanzi uwanja wa Ali hassani mwinyi kuanzia saa 12 asubuhi na kuzunguka katika viunga vya Tabora mjini na baadae kumalizikia uwanjani hapo.
Mbio hizi zimedhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo,Umoja wa Ulaya(EU),Tabora Hotel,Coca Cola,TBL na HQ .
Mgeni rasmi:Tunategemea atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
photo
EmoticonEmoticon