Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipanda mti katika
shule ya Sekondari ya Mama Salima Kikwete iliyopo Kijitonyama Jijini
Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Paul Makonda ya kupanda miti
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiongea na
wanafunzi mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shule ya
sekondari ya Mama Salima Kikwete.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akifafanua jambo
mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Salima Kikwete.
……………………………………………………………..
EVELYN MKOKOI
Kuelekea siku ya uzinduzi wa
kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam maarufu kama “mti wangu’,
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina Ameunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul
Makonda katika Jitahada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Naibu Mpina ameshiriki kwa
kutangulia kupanda mti leo katika shule ya sekondani ya Salma Kikwete
iliyopo kijitonyama jijini Dar es Saalam, ambapo wakala wa misitu nchini
wametoa miti 600 ili kukamilisha zoezi hilo katika shule hiyo ya
sekondari.
Naibu Waziri amewataka wakuu
wote wa mikoa na wilaya kuiga jitihada za Mhe. Makonda na kuacha tabia
za mazoea zilizojitokeza huko nyuma za kutoa taarifa za uwongo katika
Ofisi ya Makamu wa Rais Kuwa Miti kadhaa imepandwa lakini ki uhailisia
hakuna kilichofanyika.
Aidha ametoa wito kwa watendaji
wa serikali wanaochakachua maaagizo ya viongozi na kusema kuwa serikali
hii ipo makini hivyo kutakuwa na ufuatiliaji kwa kila Mkoa, Wilaya na
Halmashauri kwani zoezi hili la upandaji miti ni sehemu ya utekelezaji
wa ilani ya chama tawala.
“Hatutavumilia kuona miti
inakatwa ovyo, misitu inachomwa moto na viongozi wa serikali
wakilifumbia macho suala hilo.” Alisisitiza.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugezi
wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa Santos Silayo alisema, Taasisi hiyo
imetoa jumla ya miche ya miti 8000 ili kukamilisha zoezi hilo katika
jiji la Dar es Salaam, na kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa
kuonyesha mwanzo mpya na jitihada katika jiji la Dar es Salaam kwa
kupanda miti na kutunza mazingira.
Bi Jacquline Wolper Muhamasishaji
wa swala la utunzaji wa mazingira na muigizaji maarufu nchini,
akishiriki zoezi hilo, kwa kupanda miti amepongeza jitihada za mkuu wa
Mkoa Makonda kwa kuzunguka katika mashule mbalimbali jijini kuhamasisha
zoezi hilo kwa kutoa miche ya miti kadhaa.
EmoticonEmoticon