Msajili
wa Bodi ya Usajili ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB)
Arch.Jehad Abdallah akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bodi hiyo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
wa ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi,
Jijini Dar es salaam.
Mwnyekiti wa Bodi wa bodi ya Usajili ya Wabunifu
majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Arch. Ambwene Mwakyusa akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na
Wakadiriaji majenzi, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na wadau wa sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa
Ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi,
Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na wadau wa sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa
Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji
majenzi,Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi
cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi
wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati
wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji
majenzi,Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi
cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi
wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati
wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji
majenzi,Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa bodi Bodi ya Usajili
ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) mara baada ya
ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi
jijini Dar es salaam.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia
umuhimu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuungana ili waweze
kupata fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi itakayoanza hivi karibuni
hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina endelevu ya 26 ya Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi, Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Tano
imejikita katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa na itatoa kipaumbele
kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi watakaoungana ili kuwa na
nguvu ya kutekeleza miradi hiyo kwa viwango.
“Tunao
mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa miundombinu ya kisasa
mjini Dodoma, ujenzi wa makazi ya kisasa ya wananchi, vyote hivi
vinahitaji wataalamu walioungana, wenye nguvu ya kufanya kazi kwa haraka
na ubora unaokubalika”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Ameitaka
Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB),
kujitangaza na kuwatangaza wataalamu wake ili huduma zao zitumiwe na
wananchi wa ngazi zote kwa gharama nafuu.
“Shirikianeni
na vyuo vinavyofundisha fani yenu ili viongeze udahili wa wanafunzi na
kuhakikisha kazi zenu zinafanywa kisasa na kwa kuzingatia teknolojia”,
amesema Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kutoa elimu ya kutosha ili kuvutia wanafunzi
wengi kupenda kusoma fani hiyo na wale wanaofanya vizuri wawape motisha
ya kuwasomesha katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza
katika semina hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Ambwene
Mwakyusa, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga
kuhakikisha wananchi wanapata ramani za nyumba kwa bei nafuu ili kuwa na
jamii yenye makazi ya kisasa.
Naye
Msajili wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Jehad Jehad amesema takribani
Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi 1,333 pamoja na kampuni za fani
hiyo 372 zimesajiliwa na zinatoa huduma kwa mujibu wa sheria za fani
hiyo.
Amebainisha
kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha maadili ya taaluma hiyo hapa
nchini yanalindwa na atakayekiuka atafutiwa usajili na kuadhibiwa kwa
mujibu wa taratibu ya bodi hiyo.
Zaidi
ya miradi ya ujenzi 1,963 imekaguliwa na bodi hiyo katika maeneo
mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka wa 2015 lengo ikiwa ni
kuhakikisha ujenzi wowote unaofanyika nchini unakuwa na viwango bora.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
EmoticonEmoticon