Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa semina
elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye
mwaka huu.
Semina hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, itafanyika
Jumamosi Septemba 3, 2016 kwenye Ukumbi wa Hosteli za TFF zilizopo ofisi
za Makao Makuu ya shirikisho hilo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ligi hiyo ya wanawake ni ya kwanza kufanyika nchini chini ya uongozi wa Rais Jamal Malinzi kwani kabla
ya hapo hapakuwa na ligi inayohusisha mikoa mbalimbali. Shukrani za
pekee ziende kwa Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichoamua kudhamini
ligi hiyo pamoja na ile ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
TFF imeandaa semina hiyo kwa ajili ya kuwapa maelekezo kuhusu kanuni
za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwa ni
pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa
msimu wa 2016/2017 kama zilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).
Timu shiriki katika ligi ni Viva Queens ya
Mtwara, Fair Play FC ya Tanga, Panama FC ya Iringa, Mlandizi Queens ya
Pwani, Marsh Academy ya Mwanza, Baobao Queens ya Dodoma, Majengo Queens
ya Singida, Kigoma Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queen pamoja na JKT
Queens, Mburahati Queens na Evergreen Queens za Dar s Salaam.
EmoticonEmoticon