Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salamu za pongeza kwa Hani Abou-Reida kwa kuchaguliwa kwake kuwa
Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri (EFA) katika
uchaguzu mkuu uliofanyika juzi Jumanne Agosti 30, 2016 jijini Cairo.
Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Hani
Abou-Reida katika wadhifa huo ni kilelelezo cha familia ya mpira wa
miguu ya Misri kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo
sambamba na kuwa mwakilishi FIFA.
Rais Malinzi amesema ana imani na Abou-Reida kuwa ataweza kutumikia
vema nafasi hiyo sambamba na kutumikia wadhifa wa Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Abou-Reida (63) ni mjumbe wa FIFA kutoka Kanda ya Afrika Kaskazini
tangu mwaka 2009 na sasa ataongoza shirikisho la EFA kwa awamu ya kwanza
kwa miaka minne ijayo akichukua nafasi ya Galam Allam aliyeongoza EFA
tangu mwaka 2012.
Katika uchaguzi huo, wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa EFA
waliochaguliwa ni pamoja na wale wenye majina maarufu kama vile Hazem
Emam ambaye alikuwa nyota mahiri wa klabu ya Zamalek sambamba na kiungo
mkabaji mahiri wa zamani wa klabu ya Al- Ahly. Nyota hao pia walipata
kuchezea timu ya taifa maarufu kwa jina la Pharaohs.
Pia wamo Sahar El-Hawary, Hazem El-Hawary, Karam Kordi, Khaled Latif,
Seif Zaher, Mohammed Aboud El-Wafa, Ahmed Megahed a Essam Abdel-Fatah.
EmoticonEmoticon